NOGESHA UREMBO WA NYUMBA KWA KUWEKA 'PLANTER' ZA MAUA
Baadhi ya watu hujenga nyumba zao kwa kutilia mkazo urembo wa ndani pekee. Hata wakati wa kununua kiwanja husahau kufikiria na mahitaji ya nyumba kwa nje na kujikuta wananunua maeneo ambayo hayatoshelezi kujenga nyumba na kuacha eneo la wazi kwa maana ya bustani za kupumzikia, maeneo ya kuanikia nguo, kuegesha magari na hata kutengeneza urembo mwingine wa kuzunguka jengo.
Picha hii zinaonesha baadhi ya urembo wa mawe kuzunguka nyumba ukipambwa kwa maua. Hizi tunaita "planter boxes" au hata "flower boxes". Ni nzuri zaidi kwa nyumba ambayo imejengwa kwa kuwa na msingi mrefu kutokea kwenye udongo. Unaweza kuotesha maua peke yake au kuchanganya na nyasi/ukoka kutegemeana na ubunifu wako. Zaidi kwenye muonekano wa mbele ya nyumba unapoingilia.
Picha zingine zinaonesha uendelezaji wa bustani za maua na ukoka kupamba eneo la makazi. Unaweza kuiga vitu vizuri kama hivi na ukaboresha nyumbani kwako.

No comments:
Post a Comment