Header Ads

Header Ads

Mhandisi ni nani hasa kwenye ujenzi? Ipi tofauti ya Mhandisi na Mkandarasi!?


Ubunifu wa nondo na mpangilio wake, ubora wa zege na aina ya msingi wa jengo ni moja kati ya kazi wa mhandisi. Picha hii inaonesha sehemu ya msingi wa nyummba ya ghorofa moja

Kumekuwapo na mkanganyiko miongoni mwetu kuhusiana na wataalamu wa ujenzi wajuikanao kama wahandisi (Engineers) na wanataaluma wengine na hasa mkandarasi. Wapo wataalamu wengi wa ujenzi lakini kuna makosa yanafanyika na kuwafananisha watu wote kama wahandisi.
Wahandisi/(Civil and Structural Engineers)
Kawaida katika taratibu za ukamilifu wa mradi wa ujenzi kuanzia hatua ya awali kabisa, baada ya Mbunifu majengo kumaliza kazi ya kuandaa michoro yake mhadisi ndiye mtaalamu wa pili kuweka utaalamu wake.

Mara nyingi kumekuwapo na mchanganyo wa uhandisi na ukandarasi. Kuweka hili sawa kupitia blogu hii, ifahamike kuwa mhandisi ni mtaalamu mbunifu wa uimara wa jengo na mkandarasi ni mjenzi wa jengo akifanyika kazi vilivyobuniwa na wahandisi na wabunifu majengo.

Mkandarasi anaweza kuwa aidha mtu binafsi au kampuni iliyosajiliwa kufanya kazi ya ujenzi kwa kiwango fulani.


Sasa huyu anayejulikana kama Structural Engineer ndiye Mhandisi hasa na huwajibika kwa uhandisi wa ubora na uimara wa jengo kwa kufanya mahesabu ya uimara (strength), uzito, nguvu na namna vitakavyokabiliana bila kuleta madhara kwenye jengo linalotarajiwa kujengwa.


Moja ya kazi za kinadisi kwenye nyumba ya kawaida
Ni jukumu la mhandisi huyu kuandaa michoro ya uimara wa jengo kwa maana ya namna nondo na zege na hata vyuma vingine vitakavyokuwa na ukubwa wake kwa maeneo kama nguzo (column), msingi (foundation) bimu (beams), kuta, ngazi za ghorofa na slabu (slabs) kwa upande wa majumba. Halikadhalika huandaa michoro kwa ajili ya madaraja, nguzo kubwa, mabwawa n.k. 


Wakati wa ujenzi anakagua pia ubora wa bidhaa (materials) zinazotumika na namna nondo na zege zinavyotengenezwa kama vinafikia ubora unaotakiwa kama alivyobuni kimahesabu.

Inapotokea jengo limeanguka kwasababu zisizotokana na nguvu za asili kama mtetemeko ya ardhi na milipuko ya bomu kwa mfano, mhandisi ndiye hupewa majukumu ya kuchunguza sababu za kihandisi zilizopelekea hitilafu iliyosabababisha jengo kuanguka kama iivyotokea maeneo ya Kisutu Jijini Dar es Salaam miaka michache iliyopita. 

No comments: