• Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?

    Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.

  • Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?

    Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.

  • Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?

    Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Thursday, May 4, 2017

Wakandarasi 3,000 nchini wafutiwa usajili kwa kukiuka sheria.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini DODOMA wakati anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.

Makamu wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio vinginenevyo.

Makamu wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.

“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”

Kuhusu madeni ya wakandarasi, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakandarasi kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha wakandarasi.

Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.

Waziri Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na kupewa kazi.

Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.

Naye, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.

Msajili huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia 71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa wafanyakazi.

Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
IKULU- DODOMA. 4-May-2017

Thursday, March 23, 2017

WAZIRI MBARAWA AITAKA BODI YA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI (AQRB KUJITANUA ZAIDI



Judith Ferdinand, BMG

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi, nchini, imehimizwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchi jirani katika kutoa mafunzo kwa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi ili kuendane na teknolojia ya kisasa.

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, katika mafunzo endelevu ya 27 ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi yanayofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Rocky City Mall Jijini Mwanza.

Profesa Mbarawa amesema,kwa kutumia wataalamu kutoka nje ya nchi, itasaidia na kuwawezesha wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi, kubadilishana uzoefu pamoja na kuendana na soko la ushindani.

Pia amewaomba wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi,wanapopata fursa katika miradi ya ujenzi watumie elimu walionayo, kwa ajili ya maslahi ya taifa sambamba na uadilifu.

“mchina na mturiki hawawezi kujua historia ya Tanzania lakini ninyi mnaijua nchi yenu, hivyo zitumieni fursa zinapojitokeza katika kubuni michoro ambayo itadumu zaidi ya miaka mia, kulingana na historia ya nchi,katika miradi ya ujenzi,” amesema Profesa Mbarawa.

Hata hivyo ameiomba, bodi hiyo kuhakikisha inasimamia na kufuata sheria namba 4 ya mwaka 2010 katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi hasa kwa wakaguzi wa majengo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye Mkutano wa mashauriano baina ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi unaofanyika kwa siku mbili kuanzia jana, katika Ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.
Kaimu Msajili wa Bodi, Albert Munuo, akizungumza kwenye mkutano huo.

Kaimu Msajili wa Bodi hiyo, Albert Munuo, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaelimisha wataalamu na wadau wa sekta ya ujenzi kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kukabiliana na changamoto za utandawazi, ili kuchangia kukuza uchumi wa nchi, ambapo mpaka sasa yamewanufaisha wataalamu 5,556.
Mwenyekiti wa Bodi Dkt.Ambwene Mwakyusa, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Bodi, Mbunifu Majengo, Dkt.Ambwene Mwakyusa, amesema, sekta hiyo inathamini jamii inayoitumikia hivyo wametoa vifaa vya maabara za sayansi, vyenye thamani ya milioni 3, ili kuhamasisha vijana wanaosoma masomo ya sayansi, kuja kusomea ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi.
Mwenyekiti wa Bodi Dr Ambwene Mwakyusa (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) vifaa vya maabara.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema vifaa hivyo atavipeleka katika shule moja ya wasichana ya sayansi, sambamba ameishukuru bodi hiyo kupitia wataalamu wa ujenzi kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vitakua chachu kwa wanafunzi kusoma masuala ya ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi.
Wajumbe waliohudhuria mkutano huo.

MKUTANO WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAWAKUTANISHA WADAU JIJINI MWANZA


Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa, akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika Jijini Mwanza.

Judith Ferdinand, BMG
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka  nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.

Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa   mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka,  uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo  pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.

Dkt. Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa msaada wa haraka pale unapohitajika.

Pia amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442  lakini wamaotenda kazi ni wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza  kama umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.
Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani akiongea.

Kwa upande wake  Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye ndiye  mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka 2010.

Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina  wataalamu wake.

"Ikumbukwe kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi," alisema Marijani.

Naye DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi, hivyo kujua chanzo  cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka kwa wahandisi.

Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani.
Displaying Pix.JPG

Friday, January 20, 2017

MWONGOZO WA KUCHAGUA RAMANI BORA YA NYUMBA

Ramani ya nyumba-Mali ya P.Joseph

Bila shaka kila mmoja wetu anatamani kumiliki nyumba yake,na bila shaka wale ambao wamekwisha jenga wana ndoto za kujenga tena ama kuwashauri ndugu na marafiki kujenga.

Ujenzi katika sehemu kubwa ya Tanzania haufuati taratibu na sheria za ujenzi wa makazi.Zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha hili lakini kwa leo mjadala utajikita katika namna ya kuchagua ramani bora ya nyumba

Ramani ya nyumba ni dira ambayo ni kazi ya usanifu yenye kuleta picha ya uhalisia utakaofikiwa na kutarajiwa na mteja.Kazi hii hufanywa na msanifu majengo amnbaye kwa lugha ya kiingereza huitwa Architect.

Msanifu husikiliza kwa makini matarajio ya mteja na kuiweka picha ya matarajio katika mchoro (picha).Watu wengi hudhani kazi ya Architect ni kuchora tu ramani,na ndio maana wengi hudhani ni jambo rahisi.Ukweli ni kwamba kazi yake ni kusanifu mawazo ya mteja na kuyaweka kuwa halisi.Kwa maana hiyo,hii ni fani ambayo huitaji umakini na elimu ya kutosha ili kuhakikisha anasanifu jengo ambalo litafanya wanaoishi waishi wakiupata msawazo katika joto,hewa,mwanga na wawe na furaha na kupapenda wanapoishi.

Baada bya maelezo hayo sasa tujiulize je,ramani bora inazingatia mambo gani?Ijulikane kwamba nimejaribu kupitia vigezo vitakavyomfanya kila mtu aelewe

Kwa wale ambao wana mpango wa kujenga nyumba bora za kisasa,mambo
yafuatayo ni muhimu kuyazingatia unapochagua ramani bora kwa ajili ya
nyumba yako: 
Mchoro ukionesha uhusiano uliopo kati ya sehemu moja na nyingine katika eneo (site plan).Picha ni mali ya Nyumba BoraTz


1.Izingatie maono ya mteja (client)-client imaginationikiwa na maana,mteja anapaswa kupata kile anachokipenda na alichofikiri kichwani kwake eitha kwa kuona ama kwa kutarajia 

2.Iwe na uhusiano mzuri kati ya eneo na eneo (mfano sebule na dining,dining na
jiko, sebule na vyumba.

3. Izingatie matumizi bora ya ardhi kwani ardhini gharama ( iwe na mgawanyo bora kati ya eneo linalojengwa, eneo amanafasi ya kutembea (circulating space), eneo la kijana (green
zone)-ama eneo linalopandwa miti, maua na vingine vyenye kuleta uhai.Ni lazima iepuke uwepo wa sehemu zisizo na kazi (dead space)

4.Izingatie hewa na mwanga wa kutosha katika kila eneo linalotumika,nanyumba bora huzingatia hewa na mwanga wa asili na sio artificial air.(viyoyozi)

5.Izingatie uwepo wa sitiri (privacy) –ihakikishe kila mtumiajianakuwa na uhuru wa kutosha na kuepuka muingiliano

6. Izingatie kuliendeleza eneo, lisiwe mfu kwa maana ya kuliharibu ama kuondoa vitu
vya msingi ambavyo vinafanya ardhi iwe oevu/endelevu 

7. Iwe inazingatia kufikika na matumizi kwa watu wa umri wote na maumbile yote mfano wazee,walemavu. 

8. Uzingatie uzuri- iwe inavutia (appealing to eyes) na wakati Fulani mvuto wake uwe wa kipekee ama mfano mahali inapojengwapo, iwe kioo cha eneo,utamaduni na mazingira ya eneo.

9.Izingatie matumizi bora ya maji na nishati,ikihusianisha vema sehemu zinazohitaji matumizi ya maji (wet areas) na zisizohitaji maji |(dry areas), sehemu zenye kuhitaji nishati na kutoa nishati-hot areas na hivyo kurahisisha matumizi bora ya maji na nishati.Na katika zama hizi ambayo dunia inashuhudia uhaba wa maji na nishati katika nchi za Afrika,ni vizuri wasanifu majengo waanze kufikiria majengo ambayo ni rafiki katika matumizi na rafiki wa mazingira

10.Kwa nyumba ambazo ni za wakazi wengi,ni vema ikazingatia kukuza uhusiano na undugu mfano kuwe na kibaraza (verandah ya pamoja), sehemu za mapumziko za pamoja pia,ili kuhakikisha ujamaa na ushirikiano unadumishwa

 Kumbuka nyumba
utakayoijenga ni sehemu ya kudumu ( permanent structures) hivyo ni vizuri ukifahamu mapema mambo haya kabla ya kujenga kuepuka mkanganyiko wa kisaikolojia,maamuzi na uchumi. 
N:B- Nyakati hizi watu wanapenda nyumba ambazo zinaondoa kabisa uhusiano wa kijamii mfano
ukaribu na majirani,ushirikiano-nadhani ni wakati sasa wasanifu majengo Tanzania wafikirie ni jinsi gani kinachoitwa privacy kinavyoathiri ujamaa,enzi za nyerere fikra ilikuwa watu wanaotumia apartment wapike pamoja,wafue sehemu moja,lakini kwa sasa watanzania
wanafiki tofauti na labda kwa sababu hatuna falsafa inayoliunganisha taifa

CHANZO/HATIMILIKI YA STORI: UJENZIBORATZ

Kwa maswali na maoni Wasiliana nasi UJENZIBONGO ama wasiliana na UJENZIBORATZ kupitia anwani pepe nyumbaboratz@gmail.com

UCHAGUZI WA RANGI KATIKA NYUMBA

UCHAGUZI WA RANGI KATIKA NYUMBA

Rangi katika nyumba ina faida kuu mbili,zikiwa ni kuongeza nakshi (kupendezesha) na kazi ya pili ni kulinda kuta.

NYUMBA BORA TZ wamekuandalia picha hizi kuweza kuchanganua masuala ya rangi.







picha zote ni mali ya Joseph P.

Rangi za kuta zinaweza kuwekwa katika makundi mawili ya rangi msingi na rangi sekondari (upili)
Rangi msingi ni rangi ambazo hupigwa ili kuwezesha rangi upili kudumu.Hujulikana kama primer kwa lugha ya kiingereza

Makala hii fupi inalenga kushirikisha wasomaji na wale ambao wangependa kujenga kuhusu uchaguzi wa rangi.

Ni wazi kuwa kila mtu ana uchaguzi wake wa rangi,na mara nyingi kuvutia kwa rangi ni baina ya mtazamaji na maono yake.

Zipo rangi zilizopoa na zinazong'aa sana.Ni sawa na kusema rangi zinazoakisi zaidi mwanga na zile za kutunza mwanga.

CHANZO/HAKI MILIKO: NYUMBABORATZ

Saturday, December 31, 2016

Fahamu Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Ukichagua Ramani ya Nyumba Ili Usijutie Baadae

Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Ukichagua Ramani ya Nyumba Ili Usijutie Baadae

UjenziBongo


1.   Usiwe mgeni kabisa kabisa kwa kilakitu kwenye michoro ya ujenzi. Hii itakusaidia kutomuachia fundi kila kitu yakiwemo matamanio yako binafsi yafanywe na yeye, yani awaze kwa niaba yako. Angalau uwe na ufahamu mdogo waudadisi wa baadhi ya vitu kama milango, madirisha,korido, vyumba, baraza n.k ili muweze kushauriana vizurinafundi au mbunifu mpakaupate kile roho yako inataka.

2.       Fikiria maisha yako halisi na aina ya familiauliyo nayo na mtakavyoishi kwenye nyumba. Hapa namaanishalifestyle yenu. Kamaweusichague ramani tu kwa kudhani kila ramani inaendanana staili ya maisha ya kila mtu. Life style za maisha yetu hutofautiana. Unaweza kuwa unapendanyumba ya gorofa mwingine hapaendi au wewe unataka nyumba iliyojitanua chini na kona nyingi mwingine hataki.

UjenziBongo

3.       Fikiria idadi ya vyumba na nafasi unavyohitaji kulinganana ukubwa wa familia yako sasa na baadae. Jaribu kuwaza kama ndio unaishi ndani; chumba gani kiwe wapi nauweke nini, sebule iweje nauhusiano wake na jiko,dinning uwe namna gani,na mambo mengine kama hayo. Wakati mwingine kuokoa gharamakama za mfumo wa maji safi na maji taka ni muhimu kujua maeneo kama jiko, bafu na vyoo vinakaa maeneo gani.

4.       Hakikishaunadhibiti matamanio ya urembo mwingi (Architectural beauty) ili kupunguza gharamazisizo za lazima baadae. Sio kilaurembo unaouona kwa jirani ndio pekee unafaa kwako. Unaweza kushauriana na mtaalamu na kubuni features zako binafsi na nafuu. Epuka kuweka urembo ambaoutasababisha uwe na maintenance cost kubwa baadae.


UjenziBongo



5.       Hakikisha ukubwa wa rumu, korido, sebule, jiko, veranda,bafu na choo n.k aina ya fenicha na samani ulizonazoau utakazonunua kwa mahitaji yako na familia. Usingojee nyumba ikajengwa tayari ndio uanze kujaribisha vitu kama vinatoshea. Kama unatamani kitanda kikubwa hakikisha mapema kabisa ramani yako inaruhusu hilo na kuacha nafasi kiasi ya kujimwayamwaya.

6.       Kawaida nyumba huwa inapendeza na kuvutia kukaa ndani ikiwa na nafsi tofauti na kuwa imesongamana vitu kama vile ni stoo ya bidhaa. Kama wewe ni mtu wa burudani na kujumuika na marafiki nyumbani nyakati fulani fulani unaweza kuwaza kama vile yale maeneo muhimu kwa wageni wako yamejaa wakati wa kubuni ramani.

7.       Usalama ni jambo la muhimu kwako nafamilia. Nyumba yeyote lazima ikidhi mahitaji ya kiusalamakwa jingo lenyewena usalama wa matumizi na watuamiaji wake. Kuna masuala ya usalama ambayo yatasimamiwa na wataalamu,hayoni ya kiufundi Zaidi, muhimu ni kuwasisitiza yazingatiwe. Lakini pia kuna maswalaya usalama ya ninyi watuamiaji wa jingo na Zaidi watoto. Ni muhimu kujiridhisha vitu kama ngazi na reli zake, rail ya kwenye viambata, aina ya sakafu na vitu vingine ni salama kwa watumiaji na watoto hawatadhurika kwa aina ya michezo yao ilivyo.


UjenziBongo


8.       Tayari umeridhika na muonekano wa ndani na mgawanyo wavyumba, je, muonekano wan je naouakuvutia!? Kumbukama mahaliulipoamua chumba Fulani kikae,nyumba ikishajengwa huwezi kubadilishakwa mfano inatokea kwa ndani unapenda ukuta Fulani uwe na dirisha lakini kwanje unakuta dirisha likikaa hapo linaharibu umaridadi ulioutamani. Haya pia ni ya kuzingatia mwanzonikabisa kuendana na madhari ya mtaa unaoishi.

9.       Ankara. Chagua ramani na muundo sambamba na madoidoyake vinavyoendana na bajeti yako. Kama unawazia nyumba kubwa na bajeti haitoshi kukamilisha yote sasa unaweza kufikiria namnaya kupata ramani nzuri ambayo utaiendeleza taratibu huku ukiwaumehamiasehemumoja ya nyumba. Kupanga bajetinisoma jingine ambalonimeshalizungumzia kwenye Makala zilizopita.

10.   Ikiwezekana washirikishe wanafamilia wengine kuamua na kutoa ushauri kwa aina ya nyumba wanayoitamania pia. Kupitia mawazo yao unaweza kupatakilicho bora Zaidi badala yakilakitukuwa surprise tu. Mara nyingi huwa baba na mama ndiohushirikishana zaidikuamua, kama watotoni wakubwa si vibaya nao wakishirikishwa kwasababu kwa dunia ya sasa vyumba vya watotonavyo vina mahitaji yake binafsi. Ni vyemapia kujipa wakati na kupitia majarida tofauti tofauti na kujionea sampuli anuani kabla yakufikia hitimisho.



UjenziBongo
Maandaliziya materilasza ujenzi


UjenziBongo
Mafundi wakipaua nyumba,haa wanatengeneza kenji kwa ajili ya kubebea bati


KWA MAHITAJI YAKO YA USHAURI, RAMANI, WATAALAMU WA UJENZI NA UFUNZI WA AINA ZOTE USUSITE KUWASILIANA NASI KWA NAMBARI 0757718080 TUPO MOSHONO ARUSHA

Friday, December 23, 2016

Tile Flooring: Porcelain or Ceramic Tiles? Zijue tofauti hapa


Linapokuja suala la kufanya finishing ya nyumba yako unahitaji kufanya uamuzi wa aina gani ya materials utatumia kufanya finishing ya sakafu yako. Flooring (finishing ya sakafu) ziko za namna nyingi kutegemeana na materials utakayotumia kama vile VINYL, TILE,CARPET, NATURAL STONE, HARD WOOD, BAMBOO, AREA RUGS, LAMINATE na CEMENT & SAND SCREED. 

Ikumbukwe kwamba aina ya sakafu utakayochagua ina mchango mkubwa sana katika muonekano mzuri wa jengo lako. Muonekano mzuri wa jengo unatoa picha sahihi ya thamani ya jengo na kamanila biashara ya upangaji litavutia wateja zaidi. Hata hivyo sio wajenzi wote wanaweza kuchagua aina gani sahihi ya sakafu itafaa kwa majengo yao. Naomba nikupitishe taratibu kwenye makala ya leo, kwa kuanza tuangalie zaidi sakafu ya marumaru au vigae 'tile flooring'.  

Kama umeamua kutumia tiles kwenye jengo lako unalazimika kufahamu ni tiles gani utumie.  Hapo linaibuka swala la ama Marble, Ceramic tiles au Porcelain tiles. Kwa marble tiles tutaipangia toleo laken na kuijadili. Tuziangalie ceramic na porcelain tiles ambazo watu wengi na hata baadhi ya wauzaji huchukulia kama ni tiles aina moja. Kuna tofauti kidogo.

Kimsingi Porcelain na Ceramic tiles zote ni jamii moja ya tiles. Porcelain ni zao la ceramic kwa maanaya kwamba moja ni porcelain na nyingine ni non-porcelain. Sio rahisi kuzitofautisha kwa macholakini zina utofauti wa kitaalamu kwa namna zinavyotengenezwa na matumizi yake. Ieleweke kwamba bidhaa za porcelain zinapatikanakwenye vikombe, sahani n.k,hizi tunazoita sahani za udongo. Leo nitaeleza kwa ufupi kuhusu ceramic na porcelain tiles. Tusameheane pale ambapo nitashindwa kutumia nenola Kiswahili. 


Ceramic tiles ni mchanganyiko wa udongo maalumu (clay) na mchanganyiko mwingine asili. Porcelain tiles zenyewe zinatokana pia na udongo wa 'porcelain clay' lakini ni wa chembechembe ndogo sana ambazo zinachomwa kwa joto kali mno kiasi cha kufanya kaigae chake kiwe kigumu, kizito nahakipitishi maji kirahisi nahivyo kufaa kwa matumizi ya mazingira ya nje zaidi ya Ceramic tiles.

Katika kuzitofautisha kuna vitu vichache vya kufahamu ambavyo vinaweza kuwa muongozo sahihi kwako; kwamba 
  1. Ceramic tiles sioimara nazakudumu sana kwa matumizi ya nje ya jengo kwasababu zina tabia ya kunyonya sana maji kutokana na zilivyotengenezwa kwamba ninyepesina zina nafasi ya kuruhusu maji kupenya kwa urahisi. Kwa matumiziya nje hupelekea cracks baada ya muda fulanihasa kwa maeneo yenye unyevunyevu sana. 
  2. Porcelain tiles zinafaa zaidi kwa matumizi ya nje kwasababu yana kiwango kidogo cha kuruhusu maji kunyonywa nazo
  3. Porcelain tiles ni nzitozaidi na hazina nafasi wazi kuruhusu unyevunyevu kupenya kama Ceramic tiles na hivyo ni ngumu na nzito kubeba
  4. Porcelain zinadumu zaidi na zinafaa kwa maeneo ambayo ni yakupitika pitikana uzito mwingi
  5. Ceramic tiles ni laini sana kuzikata kulikoPorcelain tiles (huwazinakatwa kwakutumiamashine zinaitwa (Snap tile cutter au Wet tile saw)
  6. Na mwisho, ceramic tiles nafuu zaidi kwa maanaya gharama za kununua kuliko porcelain tiles














.

Wednesday, December 21, 2016

JE, UNAFAHAMU KUWA UBUNIFU WA JENGO HUAKISI GHARAMA HALISI ?

ujenziBongo.Co.Tz
Kitaalamu. ubunifu wa majengo hufanywa na wataalamu wanaitwa Architects ama kwa kiswahihi wabunifu majengo.

Ubunifu wa jengo ni hali ya kuumba taswira ya kufikirika na kuiweka katika hali  ya mwonekano wa kama kitu halisi, kwamba endapo ujenzi ukifanyika jengo litakuwa namna hiyo.

Ubunifu huwa ni hatua ya awali kabisa kwenye ujenzi kwa mtu ambaye tayari ana kiwanja chake na huwasilishwa kwa njia ya michoro ya kisanifu kama nilivyoeleza hapo juu, kwa kuchukua mawazo na matamanio ya mwenye kutaka kujenga na kuyaweka katika mpangiliowa mahitaji halisi kwa kuzingatia eneola ardhi lilivyo na ukubwa wake bila kusahau mazingira yanayozunguka eneohilo


Baadae utahitaji kujua gharama halisi za nyumba ya ndoto yako kulingana na ubunifu huo kwa bei ya sokoya wakatihuo. Pengine yawezekanaunahitaji kujenga baadae, nayoni sahihi kuwana mchoro na kujiandaa nao.

Hatua hii ningumukidogo na inahitaji uwe mwenye nidhamu sana katika kufikia malengo yako. Yawezekana pia umepata hela za mara moja kutokana na msihemishe zako na ukatamani ufanye uwekezaji wa nyumba. Ili kuepuka kuishia katikati ya safari, ni muhimu ukashirikisha wataalamu wabunifu na wakadiriaji gharama za ujenzi wakakushauri ni jengo gani na la ukubwa gani litatoshea pesa uliyo nayo kwamtindogani.

Kama kichwa cha habari cha somo kinavyoeleza, ubunifu ambao hutoa mwonekano halisi wa nyumba yako hutafsiri gharama halisi ya nyumba yako. Zipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika kusaidia kupunguza gharama kwenye ujenzi na wakati huohuo ukaweza kupata jengo lamuonekano wa nyumba uitakayo. Watu wengi huwa wanajenga tu kwa mazoeana kuiganyumba za majirani, hawajisumbui kufanya ubunifu wa kile ambacho nafasi zao hutamani kuwa nazo. Unaweza kusoma baadhi ya mbinu hapa za kupunguza gharama

Hata hivyo, katika hatua ya ubunifu,zipo namnatofauti zakuweza kushauriana na mbunifu majengo na kuweza ya kupunguza gharama kwa kuondoa baadhi ya mahitaji yasiyo ya lazima, kwa mfano, kupunguza idadi ya kuta za ndani, kutokuwana nafasi nyingi zisizona ulaziman.k

Kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu, unaweza kujenga nyumba bora na ya kisasa, nyumba bora ndogo inayokidhi mahitaji naukaimaliza badala ya kujenga nyumba kubwa kwa mazoea na ukashindwa kuimaliza. Amua! Unaweza! 


Njia 13 za kuweza Kuokoa Gharama Ukijenga Nyumba


Leo nakusogezea dondoo chache zinazoweka kukusaidia kupunguza gharama wakati unaanza mchakato na kufanikishaujenzi wa jengolakolakuishi
1. Nunua eneo kwa ushirikiano na ndugu, jamaa na marafiki ambao mnaaminiana, mtu mnayeweza kuishi kama majirani na kuweza kugawana eneo/kiwanja husika. 

2. Tafuta eneo ambalo halikimbiliwi na watu wengi, eneoambalo walio wengi hawafikirii kununua. Usifikirie sana kununua maeneo ya pembezoni mwa bahari, tafuta maeneo mengine yaliyotengwa kwa makazi ilikuepuka kujenga mahali pasipostahili. Viwanja vya ufukweni huwana gharamakubwa sana

3. Nunua 'material' bora lakini ya gharama nafuu kufanikisha ujenzi wako. Usinunue tu kwasababu umeona aukusikia mwingine amenunua.

4. Unaweza kukusanya mabaki ya takataka za majengo yaliyobomolewa mahali,matofali yaliyotumika n.k yatakufaa mahali katika zoezizima la ujenzi. 

5. Fikiria zaidi vitu muhimu ambavyo una hakika huwezi kuishi bila kuwa navyo. Mfano, madirisha na milango ni muhimu kwa usalama lakini jaribu kuangalia bajeti yako inatoshea nini.

6. Usijenge nyumba kubwa sana kuzidi mahitaji yako na kwa kuangalia aina ya nyumba zilizozunguka eneo lako kwasababu ikitokea unahitaji kuiuza nyumba yako makadiriohayataangalia ukubwa wanyumba bali thamani ya nyumba kulingana na mahali ulipo

7. Hakikisha kabla hujaanza ujenzi, angalau unafahamu mambo machache kuhusu gharama na na mna unaweza kupata punguzo badala ya kuwa mgeni kwa kila kitu na kuwategemea mafundiambao baadhi wanaweza kuwa sio waaminifu.

8. Tumia mafundi wazuri na ikifaa wakandarasi waliosajiliwa. Mafundi wazuri na wazoefu ni watu muhimu sana kukusaidia kupunguza gharama zisizo za lazima. 

9. Jitahidi kadiri uwezavyo kupunguza gharama za maandalizi ya site yako zisiwe kubwa sana. Weka mpango sahihi na muda wa kuanza kazi ya ujenzi ili baadhi ya shughuli zichangie gharama. 

10. Jitahidi sana kuepuka mabadiliko mengi wakati ujenzi umeanzanakuendelea kwasababu yatapelekea bajeti yako kutotoshea. 

11. Angaliakimo cha nyumba na upana wake viwe vya kawaida kuweza kuruhusu hewa nzuri ndani kwasababu kadiri nyumba inavyoenda juu zaidi na kutanuka sana ndivyo na paa litakavyohitaji gharama kubwa kulijenga. 

12. Sio lazima kuanzana sakafu za marumaru ama mbao mwanzoni kwa maanahizi zinagharama kubwa. Unaweza kufikiria sakafu ya kawaidanakuweka tile/vigae/marumaru kwenye maeneo muhimu kama jikoni,chooni na bafuni tena kwa urefu mdogo tu. Maboresho zaidi utayafanya baadae

13. Kama unafikiria kuwa na matunzio ya gari ndani, angalainamna ya kufanyaulazima huo kwa magari yote moja au kujengea kijisehemu pembeni (car shed)

Monday, December 19, 2016

Je, unaweza kutofautisha tiles za sakafu na za ukutani!? Tegua kitendawili hapa

Pichani ni ukuta wa uzio wa nyumba (fence) ukiwa umenakshiwa kwa marumaru/tiles.
Yawezekana ukaona ukuta unapendeza lakini usifahamu kama vigae/tiles vilivyotumika havikuwa sahihi.
Kwa jinsi vigae vinavyotengenezwa, hutengenezwa maalumu vikiwa na sifa maalumu kwa matumizi ya eneo maalumu. Kwa mfano, tiles za kujengea sakafuni hutengenezwa kwa kuwa na sifa (properties) zinazowezesha kufaa kwa matumizi ya sakafu kwa watumiaji kukanyaga wakitembea, halikdhalika za ukutani na ndio maana ukienda dukani unaulizia ama tiles zaukutani au za sakafu. Za uutani nazo unaweza lazimika kuulizia ama za bafuni, jikoni au maeneo mengine kwa urembo. Na za sakafuni pia hutegemeana na mahali zinapowekwa.

Kaika picha zetu hizi zinaonesha ukuta umependeza sana,lakinikama utachunguza vizuri utagundua kuwa tiles zilizotumika hapa hazikuwa maalumu kwa ukuta wa nje na baadhi ni maalumu kwa sakafu. 
Lengo la posti hiinikujaribu tu kukumbushana kukumbuka kuwa kuna tofauti ya hizi tiles kutegemeana na matumizi. Siokila wakati tutegemee mafundi pekee watuelekeze. Ni imani yangu kuwa dondoo kama hizi zitakusaidia kupata kilicho bora zaidi.

Baadae nitaweka maelezo kamili ya tilesnaainazakena wapi zitumike zipi!



Wednesday, December 14, 2016

Ujenzi wa sakafu ya mawe ya tanga yaliyokatwa kwa umbo mstatili

Jionee namna mawebapa maarufu kama "Flat Tanga Stone" yanavyoweza kutumika kutengeneza sakafu ya eneola wazi aidha kwa kuegeshea magariau watu kutembelea. Matumizi ya mawe haya yanaweza kuwa kwa 'pattern' tofauti kutegemeana na uhitaji. Unaweza weka ya rangi moja au ukachanganya na ranginyingine. 



Saturday, December 10, 2016

Angalia hapa na Ujifunze Umaridadi mwingine kwa Uzio wa Nyumba yako

Kadiri teknolojiainavyokuwa ndivyo na ubunifu wa mapambo ya nyumba huongezeka. Leo nakusogezeapicha hizi mbili zikionesha urembo mzuri na geti lililopambwa vizuri kuanzia muundo wake na finishin zilizvyofanywa.

Picha ya chini ni rough plaster kwenye ukuta wa tofali kama inavyoonekana. Ukihitaji ufundi wa namna hii ususite kuwasiliana nasi kwa nambari 0757718080 na kuona namna ya kusaidiana kupata kilicho bora! Karibu sana




Saturday, November 26, 2016

UKO DAR!? UNAHITAJI MAGETI YA KISASA YA KUSLIDE? WAONE UZ METAL WORKS

MAGETI YA KISASA YA KUSLIDE @ UZ METAL WORKS

Uwapo Dar es Salaam mjini usiwaze wapi utapata mageti mazuri ya kuslide.gharama zinaanzia sh 1.6m na kuendelea .Tuko Mwenge ITV na Goba Tatedo Dsm. Simu 0786808707

Saturday, November 19, 2016

Nini suluhu ya ujenzi holela katika miji yetu?




Ukitembelea maeneo mengi  ya miji  yanayokua utakuta nyumba za makazi zimejengwa kwa kusongana sana kiasi cha kushindwa kuruhusu huduma za dharura kama gari la wagonjwa ama la kuzimia moto kutoweza kufika kila mahali.

Hatari ya moto pia huwa kubwa zaidi kuambikiza nyumba nyingine zilizo jirani  kutokana na zilivyosongana.

Kama picha  inavyoonesha ndivyo ambavyo  maeneo mengi  ya makazi yamejengeka. Hakuna uhuru  wa kupita  na hata utambuzi wa nyumba unakuwa mgumu.

Kadiri miji  inavyokuwa na kuhitaji maboresho ndivyo ambavyo  adha  ya kusongamana huku inavyoonekana. Kwa mfano, upanuzi na uboreshaji wa barabara kwa viwango vya lami unapata changamoto ya kukosa eneo la kutosha kujenga barabara nzuri na huduma za waenda kwa miguu.

Harakaharaka, haya yanatokana na maeneo hayo kutopimwa na watu pengine  kutoka na na kipato duni wanaamua kujijengea kadiri anavyopata kijieneo.

Unadhani kuna suluhisho zaidi tofauti na maeneo kuwa yamepimwa na wananchi kutakiwa kujenga kwa kufuata mpango  wa mji!?