Nini suluhu ya ujenzi holela katika miji yetu?
Ukitembelea maeneo mengi ya miji yanayokua utakuta nyumba za makazi zimejengwa kwa kusongana sana kiasi cha kushindwa kuruhusu huduma za dharura kama gari la wagonjwa ama la kuzimia moto kutoweza kufika kila mahali.
Hatari ya moto pia huwa kubwa zaidi kuambikiza nyumba nyingine zilizo jirani kutokana na zilivyosongana.
Kama picha inavyoonesha ndivyo ambavyo maeneo mengi ya makazi yamejengeka. Hakuna uhuru wa kupita na hata utambuzi wa nyumba unakuwa mgumu.
Kadiri miji inavyokuwa na kuhitaji maboresho ndivyo ambavyo adha ya kusongamana huku inavyoonekana. Kwa mfano, upanuzi na uboreshaji wa barabara kwa viwango vya lami unapata changamoto ya kukosa eneo la kutosha kujenga barabara nzuri na huduma za waenda kwa miguu.
Harakaharaka, haya yanatokana na maeneo hayo kutopimwa na watu pengine kutoka na na kipato duni wanaamua kujijengea kadiri anavyopata kijieneo.
Unadhani kuna suluhisho zaidi tofauti na maeneo kuwa yamepimwa na wananchi kutakiwa kujenga kwa kufuata mpango wa mji!?
No comments:
Post a Comment