Header Ads

Header Ads

Je, Unaweza Kutofautisha Kati ya Lenta na Bimu (lintel & beam) kwenye nyumba!? Soma hapa

Watu wengi huwa wanapata ugumu wa kutofautisha kati ya "beam"au bimu na "lintel" au lenta kwenye ujenzi wa nyumba. Wapo baadhi ya mafundi pia wanajichanganya katika hili. Baada ya kusoma hapa na kuangalia picha hizi natumaini utakuwa umeweza kujua tofauti halisi. 

Kabla ya kuangalia tofauti zake, bimu ama leta zinaweza kujegwa kwenye jengo kwa kutumia 'material' za  aina tofauti. Hebu kwanza tuangalie kila kimojani kitu gani ndipo tuweze kuona tofauti baina yao..

Lintel ama lenta ni nini!? 

Lenta ni memba ya jengo ambayo huwekwa juu ya uwazi wa ama mlango au dirisha na kadhalika kama picha hizi zinavyoonesha. Unene wa lenta mara nyini huwa sawa na unene wa ukuta husika, na kina chake (depth) kinaweza kuwa mm 100, 150 au zaidi kidogo.

Lenta zipo za aina nyingi kama nilivyoeleza awali, kama vile 
(a) Lenta ya zege na nondo
(b) Lenta ya matofali ya ya kawaida au ya kuchoma
(c) Lenta ya mawe
(d) Lenta ya mbao, ama
(e) Lenta ya chuma

Bimu (beam) ni nini kwenye nyumba?
Bimu ni memba ya jengo inayobeba uzito unaosambaa kufuata mzunguko wajengo, na hutofautishwa kutegemeana na vitu kama
(a) Upana wa ndani kwa ndani kutoka kwenye egemeo moja na jingine la ukuta
(b) kiunganishio cha kubeba kenchi au sakafu (floor) zinazoning'inia
(c) Kama Girders, ambapo zinafanya kazi kama jukwaa la kubebea sakafu (vibeba uzito)
(d) Spandrels. Hizi ni bimu ambazo ziko kwanje usawa wa floor zikiwa mhsusikubeba sehemu ya uzito/mzigo wa sakafu kupeleka ukuta wanje. 
(e) Dead load beams, hizi huwa mahsusi kubeba mzigo wote wa jengo lenyewe na kuupeleka kwenye nguzo za jengo (columns kwa ajili ya kuushusha ardhini
(f) Live load beama, ambazo hubeba uzito unaotokana na nguvu ya nje inayoshukia kwenye jengo

Yote kwa yote, kwa kawaida bimu ziko za aina zifuatazo
(a) Simply supported beam 
(b) Cantilever beam (iliyoshikiliwa upande mmoja)
(c) Rigidly fixed beam (iliyosikiliwa vizuri)
(d) Over hanging beam (inayoning'inia)

Kuhitimisha somo letu, kwa lugha rahisi zaidi, bimu inajitofautisha na lenta kwa maana kwamba yenyewe huwana kazi kubwa ya kubeba uzito kwenye jengo na wakati mwingine huzunguka jengo zima wakati lenta yenyewe huwekwa juu ya uwazi wa mlango ama dirisha kwaajili ya kufanya uwazi huo uwepo na kwajuu yake ukuta uendelee. Pichanini mbao zimetengenezwa kuwezesha kutengeneza bimu ya zege na nondo kuzunguka nyumba nzima. 












No comments: