-
Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?
Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.
-
Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?
Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.
-
Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?
Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.
Thursday, May 4, 2017
Wakandarasi 3,000 nchini wafutiwa usajili kwa kukiuka sheria.
Thursday, March 23, 2017
WAZIRI MBARAWA AITAKA BODI YA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI (AQRB KUJITANUA ZAIDI
MKUTANO WA BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI WAWAKUTANISHA WADAU JIJINI MWANZA
Maofisa wa Jeshi la Polisi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambyo ni Mwanza, Kigoma, Kagera,Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, wamenufaika na elimu kuhusu sheria namba 4 ya mwaka 2010, kwenye sekta ya ujenzi.
Elimu hiyo imetolewa leo katika ufunguzi wa mkutano wa mashauriano kati ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi,Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashitaka, uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi Mbunifu Majengo Dkt. Ambene Mwakyusa amesema, malengo ya mkutano huo ni kubadilishana uzoefu,ili kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 4 ya mwaka 2010 bila vikwazo pamoja na kujitambulisha kwa wadau,shughuli za bodi,kuelimisha umuhimu wa kuwatumia wataalamu katika shughuli za ujenzi.
Dkt. Mwakyusa amesema, wameona watumie utaratibu wa kuelimisha Maofisa wa Jeshi la Polisi na ofisi ya DPP,ili waelewe sheria hiyo na waweze kutoa msaada wa haraka pale unapohitajika.
Pia amesema,Bodi imesajili wataalamu 1442 lakini wamaotenda kazi ni wacheche kutokana na wengine kuwa walimu vyuoni, hivyo wameona jeshi la Polisi ndio wenye uwezo wa kuwasaidia pale ujenzi unapoanza kama umefuata taratibu za kiserikali kwa kufatilia stika na vibao vinavyobandika kama ilivyo kwa bima na leseni kwa dereva.
Kwa upande wake Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo Nsato Marijani ambaye ndiye mgeni rasmi amesema, jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Bodi hiyo, katika usimamizi wa sheria pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa mtu yoyote atakayeenda kinyume na maelezo ya Sheria namba 4 ya mwaka 2010.
Aidha ameiomba, Bodi hiyo kutoa ushirikiano hasa pale ushahidi unapotakiwa kwa muda muafaka,kwani kila fani ina wataalamu wake.
"Ikumbukwe kila fani inawataalamu wake, hivyo ushirikiano wenu katika kutoa taarifa za kitaalamu utasaidia sana wataalamu wa jeshi la Polisi kuchukua hatua syahiki kwa wakati na wepesi," alisema Marijani.
Naye DPP Mganga amesema, siyo wapelelezi wote wana taaluma ya uhandisi, hivyo kujua chanzo cha jengo kubomoka mpaka wapate ushirikiano kutoka kwa wahandisi.
Kadhalika amesema,mtu yoyote atakayefanya kosa katika ujenzi na kuwepo kwa ushahidi atafikishwa mahakamani.
Friday, January 20, 2017
MWONGOZO WA KUCHAGUA RAMANI BORA YA NYUMBA
| Ramani ya nyumba-Mali ya P.Joseph |
![]() |
| Mchoro ukionesha uhusiano uliopo kati ya sehemu moja na nyingine katika eneo (site plan).Picha ni mali ya Nyumba BoraTz |
UCHAGUZI WA RANGI KATIKA NYUMBA
UCHAGUZI WA RANGI KATIKA NYUMBA
NYUMBA BORA TZ wamekuandalia picha hizi kuweza kuchanganua masuala ya rangi.
![]() |
![]() |
| picha zote ni mali ya Joseph P. |
Rangi za kuta zinaweza kuwekwa katika makundi mawili ya rangi msingi na rangi sekondari (upili)
Rangi msingi ni rangi ambazo hupigwa ili kuwezesha rangi upili kudumu.Hujulikana kama primer kwa lugha ya kiingereza
Makala hii fupi inalenga kushirikisha wasomaji na wale ambao wangependa kujenga kuhusu uchaguzi wa rangi.
Ni wazi kuwa kila mtu ana uchaguzi wake wa rangi,na mara nyingi kuvutia kwa rangi ni baina ya mtazamaji na maono yake.
Zipo rangi zilizopoa na zinazong'aa sana.Ni sawa na kusema rangi zinazoakisi zaidi mwanga na zile za kutunza mwanga.
Saturday, December 31, 2016
Fahamu Mambo 10 Muhimu ya Kuzingatia Ukichagua Ramani ya Nyumba Ili Usijutie Baadae
![]() |
| Maandaliziya materilasza ujenzi |
![]() |
| Mafundi wakipaua nyumba,haa wanatengeneza kenji kwa ajili ya kubebea bati |
Friday, December 23, 2016
Tile Flooring: Porcelain or Ceramic Tiles? Zijue tofauti hapa
- Ceramic tiles sioimara nazakudumu sana kwa matumizi ya nje ya jengo kwasababu zina tabia ya kunyonya sana maji kutokana na zilivyotengenezwa kwamba ninyepesina zina nafasi ya kuruhusu maji kupenya kwa urahisi. Kwa matumiziya nje hupelekea cracks baada ya muda fulanihasa kwa maeneo yenye unyevunyevu sana.
- Porcelain tiles zinafaa zaidi kwa matumizi ya nje kwasababu yana kiwango kidogo cha kuruhusu maji kunyonywa nazo
- Porcelain tiles ni nzitozaidi na hazina nafasi wazi kuruhusu unyevunyevu kupenya kama Ceramic tiles na hivyo ni ngumu na nzito kubeba
- Porcelain zinadumu zaidi na zinafaa kwa maeneo ambayo ni yakupitika pitikana uzito mwingi
- Ceramic tiles ni laini sana kuzikata kulikoPorcelain tiles (huwazinakatwa kwakutumiamashine zinaitwa (Snap tile cutter au Wet tile saw)
- Na mwisho, ceramic tiles nafuu zaidi kwa maanaya gharama za kununua kuliko porcelain tiles.
.
Wednesday, December 21, 2016
JE, UNAFAHAMU KUWA UBUNIFU WA JENGO HUAKISI GHARAMA HALISI ?
Ubunifu wa jengo ni hali ya kuumba taswira ya kufikirika na kuiweka katika hali ya mwonekano wa kama kitu halisi, kwamba endapo ujenzi ukifanyika jengo litakuwa namna hiyo.
Ubunifu huwa ni hatua ya awali kabisa kwenye ujenzi kwa mtu ambaye tayari ana kiwanja chake na huwasilishwa kwa njia ya michoro ya kisanifu kama nilivyoeleza hapo juu, kwa kuchukua mawazo na matamanio ya mwenye kutaka kujenga na kuyaweka katika mpangiliowa mahitaji halisi kwa kuzingatia eneola ardhi lilivyo na ukubwa wake bila kusahau mazingira yanayozunguka eneohilo
Baadae utahitaji kujua gharama halisi za nyumba ya ndoto yako kulingana na ubunifu huo kwa bei ya sokoya wakatihuo. Pengine yawezekanaunahitaji kujenga baadae, nayoni sahihi kuwana mchoro na kujiandaa nao.
Hatua hii ningumukidogo na inahitaji uwe mwenye nidhamu sana katika kufikia malengo yako. Yawezekana pia umepata hela za mara moja kutokana na msihemishe zako na ukatamani ufanye uwekezaji wa nyumba. Ili kuepuka kuishia katikati ya safari, ni muhimu ukashirikisha wataalamu wabunifu na wakadiriaji gharama za ujenzi wakakushauri ni jengo gani na la ukubwa gani litatoshea pesa uliyo nayo kwamtindogani.
Kama kichwa cha habari cha somo kinavyoeleza, ubunifu ambao hutoa mwonekano halisi wa nyumba yako hutafsiri gharama halisi ya nyumba yako. Zipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika kusaidia kupunguza gharama kwenye ujenzi na wakati huohuo ukaweza kupata jengo lamuonekano wa nyumba uitakayo. Watu wengi huwa wanajenga tu kwa mazoeana kuiganyumba za majirani, hawajisumbui kufanya ubunifu wa kile ambacho nafasi zao hutamani kuwa nazo. Unaweza kusoma baadhi ya mbinu hapa za kupunguza gharama
Hata hivyo, katika hatua ya ubunifu,zipo namnatofauti zakuweza kushauriana na mbunifu majengo na kuweza ya kupunguza gharama kwa kuondoa baadhi ya mahitaji yasiyo ya lazima, kwa mfano, kupunguza idadi ya kuta za ndani, kutokuwana nafasi nyingi zisizona ulaziman.k
Kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu, unaweza kujenga nyumba bora na ya kisasa, nyumba bora ndogo inayokidhi mahitaji naukaimaliza badala ya kujenga nyumba kubwa kwa mazoea na ukashindwa kuimaliza. Amua! Unaweza!
Njia 13 za kuweza Kuokoa Gharama Ukijenga Nyumba
Monday, December 19, 2016
Je, unaweza kutofautisha tiles za sakafu na za ukutani!? Tegua kitendawili hapa
Yawezekana ukaona ukuta unapendeza lakini usifahamu kama vigae/tiles vilivyotumika havikuwa sahihi.
Kwa jinsi vigae vinavyotengenezwa, hutengenezwa maalumu vikiwa na sifa maalumu kwa matumizi ya eneo maalumu. Kwa mfano, tiles za kujengea sakafuni hutengenezwa kwa kuwa na sifa (properties) zinazowezesha kufaa kwa matumizi ya sakafu kwa watumiaji kukanyaga wakitembea, halikdhalika za ukutani na ndio maana ukienda dukani unaulizia ama tiles zaukutani au za sakafu. Za uutani nazo unaweza lazimika kuulizia ama za bafuni, jikoni au maeneo mengine kwa urembo. Na za sakafuni pia hutegemeana na mahali zinapowekwa.
Kaika picha zetu hizi zinaonesha ukuta umependeza sana,lakinikama utachunguza vizuri utagundua kuwa tiles zilizotumika hapa hazikuwa maalumu kwa ukuta wa nje na baadhi ni maalumu kwa sakafu.
Baadae nitaweka maelezo kamili ya tilesnaainazakena wapi zitumike zipi!
Wednesday, December 14, 2016
Ujenzi wa sakafu ya mawe ya tanga yaliyokatwa kwa umbo mstatili
Saturday, December 10, 2016
Angalia hapa na Ujifunze Umaridadi mwingine kwa Uzio wa Nyumba yako
Picha ya chini ni rough plaster kwenye ukuta wa tofali kama inavyoonekana. Ukihitaji ufundi wa namna hii ususite kuwasiliana nasi kwa nambari 0757718080 na kuona namna ya kusaidiana kupata kilicho bora! Karibu sana
Saturday, November 26, 2016
UKO DAR!? UNAHITAJI MAGETI YA KISASA YA KUSLIDE? WAONE UZ METAL WORKS
Saturday, November 19, 2016
Nini suluhu ya ujenzi holela katika miji yetu?
Ukitembelea maeneo mengi ya miji yanayokua utakuta nyumba za makazi zimejengwa kwa kusongana sana kiasi cha kushindwa kuruhusu huduma za dharura kama gari la wagonjwa ama la kuzimia moto kutoweza kufika kila mahali.
Hatari ya moto pia huwa kubwa zaidi kuambikiza nyumba nyingine zilizo jirani kutokana na zilivyosongana.
Kama picha inavyoonesha ndivyo ambavyo maeneo mengi ya makazi yamejengeka. Hakuna uhuru wa kupita na hata utambuzi wa nyumba unakuwa mgumu.
Kadiri miji inavyokuwa na kuhitaji maboresho ndivyo ambavyo adha ya kusongamana huku inavyoonekana. Kwa mfano, upanuzi na uboreshaji wa barabara kwa viwango vya lami unapata changamoto ya kukosa eneo la kutosha kujenga barabara nzuri na huduma za waenda kwa miguu.
Harakaharaka, haya yanatokana na maeneo hayo kutopimwa na watu pengine kutoka na na kipato duni wanaamua kujijengea kadiri anavyopata kijieneo.
Unadhani kuna suluhisho zaidi tofauti na maeneo kuwa yamepimwa na wananchi kutakiwa kujenga kwa kufuata mpango wa mji!?



































