-
Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?
Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.
-
Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?
Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.
-
Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?
Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.
Saturday, November 26, 2016
UKO DAR!? UNAHITAJI MAGETI YA KISASA YA KUSLIDE? WAONE UZ METAL WORKS
Saturday, November 19, 2016
Nini suluhu ya ujenzi holela katika miji yetu?
Ukitembelea maeneo mengi ya miji yanayokua utakuta nyumba za makazi zimejengwa kwa kusongana sana kiasi cha kushindwa kuruhusu huduma za dharura kama gari la wagonjwa ama la kuzimia moto kutoweza kufika kila mahali.
Hatari ya moto pia huwa kubwa zaidi kuambikiza nyumba nyingine zilizo jirani kutokana na zilivyosongana.
Kama picha inavyoonesha ndivyo ambavyo maeneo mengi ya makazi yamejengeka. Hakuna uhuru wa kupita na hata utambuzi wa nyumba unakuwa mgumu.
Kadiri miji inavyokuwa na kuhitaji maboresho ndivyo ambavyo adha ya kusongamana huku inavyoonekana. Kwa mfano, upanuzi na uboreshaji wa barabara kwa viwango vya lami unapata changamoto ya kukosa eneo la kutosha kujenga barabara nzuri na huduma za waenda kwa miguu.
Harakaharaka, haya yanatokana na maeneo hayo kutopimwa na watu pengine kutoka na na kipato duni wanaamua kujijengea kadiri anavyopata kijieneo.
Unadhani kuna suluhisho zaidi tofauti na maeneo kuwa yamepimwa na wananchi kutakiwa kujenga kwa kufuata mpango wa mji!?
Wednesday, November 16, 2016
Je, Unaweza Kutofautisha Kati ya Lenta na Bimu (lintel & beam) kwenye nyumba!? Soma hapa
Tuesday, November 15, 2016
KUTANA NA MBUNIFU MAJENGO EDWARD KAYOMBO HAPA! ISHI KATIKA NDOTO YAKO

Thursday, November 3, 2016
Waziri Lukuvi - Asilimia 85 ya Ardhi nchini haijapimwa,Watu wengi wanaendelea kuishi katika makazi holela
Amesema kuwa serikali inapoteza mapato kutokana na kuwa na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa.Lukuvi amesema wapimaji wa sekta binafsi wamekuwa wakifanya vizuri kuliko wale ambao wameajiliwa na serikali.
Amesema lazima kuondokana na mfumo wa hati kwenye karatasi na kuingia katika mfumo wa kieletroniki katika kusaidia wananchi kudhulumiwa ardhi kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu.
Waziri Lukuvi amesema ni marufuku kwa wapimaji ardhi walioajiliwa na serikali kuwa kampuni za upimaji wa ardhi ili kuondokana na mgongano wa kimasilahi. Amesema katika miaka 10 ijayo kuwa kila mtu kuwa hati na kiwanja au shamba kiwe kimepimwa.Lukuvi amesema katika kuondoa migogoro ya wafugaji ni kuondokana na uchungaji wa mifugo.
Amesema kufika mwishoni mwa mwaka huu wawe wamepima ardhi viwanja 400.Nae Rais IST, Martins Chodata amesema kuwa watashirikiana na serikali katika masuala ya upimaji ardhi.Amesema wapo baadhi ya wapimaji ardhi hawana maadili na kusababisha kuwepo migogoro.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa moja ya vifaa vinavyotumika katika upimaji wa Ardhi mapema leo katika Mkutano mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akipewa maelezo jinsi mambo yalivyobadirika katika mfumo wa Kidigitali.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiwa amebeba moja ya kifaa kinachotumika katika upimaji.
Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akionyeshwa kifaa cha kisasa kinachotumika katika upimaji.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.
Wapimaji wa Ardhi wakiwa katika mkutano Mkuu na Kongamano la Wapimaji Ardhi.