MKUTANO WA CRB 2016: RAIS MAGUFULI AHIMIZA WAZAWA KUCHANGAMKIA FURSA UJENZI BOMBA LA MAFUTA KWENDA UGANDA
Kwa mujibu wa mtandao wa MillardAyo.com Rais Magufuli amenukuliwa akieleza hivi ”Sina uhakika kwamba mmejipangaje wakandarasi wa Tanzania katika kuhakikisha hiyo kazi mnaipata ya kujenga bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga ..... Nitasikitika sana kilometa zote 1,410 pasiwepo mkandarasi hata mmoja wa kutoka Tanzania, wenzetu wanajipanga, na ninavyoona wakandarasi wa Tanzania wameendelea sana, lakini nashindwa kuelewa kuna tatizo gani linatufanya kutojua changamoto zinazotukabili.... tumejipanga kujenga reli ya kati (Standard Gauge) kwenye bajeti ya mwaka huu tunaanza na kilometa 100, lakini kuna fedha nyingine zitatolewa na serikali ya China, tutajenga zaidi ya kilometa 1,200 itakayounganisha Mwanza, Kigoma, Burundi na Rwanda. Wakandarasi wa Tanzania mmejipangaje?''
.Rais Magufuli akihutubia wakandarasi.
.
Rais Magufuli na Waziri Mbarawa wakifanya ukaguzi wa baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
.
Rais Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi
No comments:
Post a Comment