• Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?

    Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.

  • Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?

    Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.

  • Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?

    Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Friday, May 27, 2016

Kutoka CRB: Makandarasi 4572 Wafutiwa Leseni Nchini



Bodi ya Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya mwaka 1997.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw. Rhoben Nkhori wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Nkhori amesema kuwa katika jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi ilikagua miradi 2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na asilimia 68.5 haikuwa na kasoro.

Ameongeza kuwa miradi mingine ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi waliosajiliwa, kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio na miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana na upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Bwana Nkhori amesema kuwa kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye thamani ya shilingi trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na Makandarasi wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.

Licha ya mafanikio hayo CRD ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za kugushi wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya wataalam, kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao, waendelezaji kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya makandarasi kushindwa kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa amemwomba Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu nchini ili kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani sisi tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la ajira,”alisema Bi Ngimbwa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi wazawa lakini akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Mkutano huu pamoja na mamabo mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”

'FLY OVER' SABA KUJENGWA DAR: PROF. MBARAWA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mkakati wa kupunguza msongamano katikati ya jiji la Dar es salaam leo ofsini kwake. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo (sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga.
Meneja Mradi wa Daraja la Nyerere kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. Karim Mattaka, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), wakati alipotembelea daraja hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akitoka kukagua moja ya Ofisi zilizopo katika daraja la Nyerere. Kushoto ni Msimamizi wa daraja hilo kutoka NSSF Gerald Sondo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa daraja la Nyerere kutoka NSSF Gerald Sondo (kushoto)kuhusu mfumo wa tozo za magari darajani hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo ya ujenzi wa bomba la kupima mafuta (flow meter) kutoka kwa Fundi mitambo wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Simon Dottto (kushoto).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mafundi mitambo wanaojenga bomba la kupima mafuta (flow meter) kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akisikiliza maoni kutoka kwa wakazi wa Kigamboni wakati wakisubiri kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (mwenye shati jeupe), akiwa pamoja na wasafiri wanaoutumia kivuko cha MV Kigamboni leo jijini Dar es salaam.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeanza mazungumzo na Kampuni ya MABE BRIDGE ya Uingereza kwa ajili ya kujenga barabara za juu (fly over) saba katikati ya jiji la Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema mazungumzo kuhusu ujenzi huo yako katika hatua nzuri na kwa kuanzia zitajengwa fly over nne za watembea kwa miguu na tatu za magari.

Amesema Fly over hizo zitazojengwa zitatumia miezi mitatu hadi sita kukamilika kwakwe na zitagharamiwa na fedha za ndani za Serikali ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza Desemba mwaka huu.

“Wataalamu wanaendelea kubaini maeneo yatakayojengwa fly over hizo ikiwemo eneo la Mwenge ambalo tayari wataalamu wamekubali kujenga fly over moja ya magari”, amesema Prof. Mbarawa.

Hatua hiyo ni mkakati wa Serikali kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam unaogharimu fedha nyingi kutokana na watu kupoteza muda mwingi barabarani.

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua maendeleo ya utoaji huduma katika Daraja la Nyerere na kuagiza vitengenezwe vitambulisho vya msimu vitakavyowawezesha watumiaji wa daraja kulipa tozo kwa miezi sita au mwaka ili kupunguza msongamano wa kulipa kila siku.

“Hakikisheni mnatengeneza na kuuza kadi za kuvukia katika daraja sehemu mbalimbali ili kuwawezesha watumiaji kupata huduma hiyo kabla ya kufika darajani”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha amemtaka Mtendaji Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo kuhakikisha tozo zinakusanywa inavyostahili na kupanga njia maalumu za kupita magari makubwa na madogo ili kuwezesha huduma ya kupita darajani iwe ya haraka.

“Magari yote yanayopita katika daraja hili yakiwemo ya Serikali ni lazima yalipe tozo inayostahili isipokuwa yale yenye vibali maalumu yakiwemo ya Jeshi la Wananchi, Zimamoto, Polisi, na yanayobeba wagonjwa (Ambulance)”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amesisitiza umuhimu wa wananchi kutunza na kulilinda Daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu na kusisitiza adhabu kali kwa wataohujumu miundombinu yake.

Naye Mtendaji Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo amemueleza Waziri Mbarawa kuwa chanagamoto zinazowakabili kwa sasa ni kubaini magari yenye vibali maalumu, malalamiko ya magari ya abiria (daladala), uelewa mdogo wa matumizi ya daraja na mazoea ya kupita bila ya kulipa tozo.

Zaidi ya magari elfu nane hadi elfu kumi na tatu hupita katika daraja hilo kwa siku huku watembea kwa miguu, baiskeli wakipita bila kulipa tozo.

MKUTANO WA CRB 2016: RAIS MAGUFULI AHIMIZA WAZAWA KUCHANGAMKIA FURSA UJENZI BOMBA LA MAFUTA KWENDA UGANDA

.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefungua mkutano wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa wakandarasi (CRB) kwa mwaka 2016 unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa wakandarasi hao kujipanga ipasavyo ili waweze kupata zabuni katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi itakayofanywa hapa nchini ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga hapa Tanzania, Ujenzi wa Reli ya Kati na Ujenzi wa Viwanda. Tukio hilo limefanyika leo Alhamisi ya Mei 26, 2016.
Kwa mujibu wa mtandao wa MillardAyo.com Rais Magufuli amenukuliwa akieleza hivi Sina uhakika kwamba mmejipangaje wakandarasi wa Tanzania katika kuhakikisha hiyo kazi mnaipata ya kujenga bomba kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga ..... Nitasikitika sana kilometa zote 1,410 pasiwepo mkandarasi hata mmoja wa kutoka Tanzania, wenzetu wanajipanga, na ninavyoona wakandarasi wa Tanzania wameendelea sana, lakini nashindwa kuelewa kuna tatizo gani linatufanya kutojua changamoto zinazotukabili.... tumejipanga kujenga reli ya kati (Standard Gauge) kwenye bajeti ya mwaka huu tunaanza na kilometa 100, lakini kuna fedha nyingine zitatolewa na serikali ya China, tutajenga zaidi ya kilometa 1,200 itakayounganisha Mwanza, Kigoma, Burundi na Rwanda. Wakandarasi wa Tanzania mmejipangaje?'' 
.
.Rais Magufuli akihutubia wakandarasi.
.
.
.
Rais Magufuli na Waziri Mbarawa wakifanya ukaguzi wa baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
.
.
.
Rais Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano
.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi
.

PICHA ZOTE NA MILLARDAYO.COM.

Saturday, May 21, 2016

Cement mpya maalum kwa uashi "Tembo Fundi" yaingia sokoni

Mfano wa sebule na eneo la jiko vilivyonakshiwa vizuri. Picha na mtandao

Kampuni ya sarujli ya Lafarge Tanzania imezindua simenti maalumu iliyopewa jina la  Tembo Fundi  ambayo ni  kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni pamoja na upigaji plasta ukutani, kusakafia, kujengea matofali, na kupangilia marumaru.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Ilse Boshoff, simenti hii imetengenezwa maalumu kuwezesha shughuli za ujenzi kuwa bora zaidi.

Tembo Fundi  imetengeneza kuwa rahisi kuitumia katika kupiga plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo itamchukua mwashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta, huku ikitumia maji kidogo na kuwa na ubora mzuri.


Mfano wa nyumba iliyopigwa plasta kwa simenti ya kawaida/ya jumla