-
Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?
Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.
-
Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?
Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.
-
Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?
Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.
Tuesday, October 23, 2012
Monday, October 8, 2012
Taswira Za Ujenzi Wa Stendi Kuu Ya Mabasi Kigoma Unaendelea
Taswira: Makamu wa Rais Dkt. Bilal Akihitimisha Matembezi ya Wahandisi jana
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal,akimkabidhi cheti, Mhandisi Grace Beo, kutoka Kampuni ya Temesa ICT Engineer, akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Wahandisi (Local Engineers) baada ya kuhitimisha matembezi hayo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Daar es Salaam leo, Oktoba 7, 2012.
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
Wednesday, September 5, 2012
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AZINDUA UJENZI WA JENGO KUU LA ELIMU HURIA NA MASAFA
Picha ya pamoja, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa pamoja na Mama Maria Nyerere aliyekuwepo katika uzinduzi huo.
Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa kama linavyoonekana ambalo ujenzi wake umezinduliwa leo 5/9/2012 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Kawambwa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk.Kawambwa akifurahi baada ya kuzindua ujenzi wa Jengo kuu la Elimu Huria na Masafa leo huku Mama Maria Nyerere akimpongeza.
Mama Maria Nyerere,Mhe.Dk.Kawambwa wakifurahia jambo na wageni wengine baada ya uzinduzi wa Jengo
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Prof.Tolly Mbwette akitoa maelezo ya awali kuhusiana na ujenzi wa Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa kwa Wageni waalikwa katika uzinduzi waliokuja kushuhudia Uzinduzi huo leo 5/9/2012 katika Ofisi za Muda za Chuo Kinondoni,Dar es Salaam.
SOURCE: RUNDUGAI BLOG
ROOF CONSTRUCTION FOR RESIDENTIAL HOUSES
Kenji (truses) zikiwa zimeshikizwa kwenye bimu ya zege (reiforced concrete beam) kutengeneza paa la nyumba mtindo wa (pitch) kama linavyoonekana kwa kutokea ndani. Bolt na nati ndizo zimetumika kushikilia bimu zikikazwa kwa kucomewa (welding). Tie beam wametumia mbao mbili kwa uimara zaidi. Kwa kawaida kenji linaweza kuwa la chuma au mbao kutegemeana na uimara unaohitajika. Mbao za kenji zina ukubwa wa 150x50mm.
Mbao ulalo kwa saizi ya unene wa 50x50mm zimewekwa kwa upana unaofanana. kwa kitaalamu mbao hizi huitwa purlins.
Vigae hupangwa kimoja kimoja kwa kufuata purlins zilivyojipanga
Monday, September 3, 2012
WAHANDISI KUADHIMISHA SIKU YAO MWEZI HUU, JIJINI DAR
Mhandisi Prof. Ninatubu Lema
Na Aron Msigwa – MAELEZO.
Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini imewataka watanzania kutumia huduma za wakandarasi waliosajiliwa kisheria ili kuepuka kupata maafa na hasara inayotokana na ujenzi hafifu usiokidhi viwango.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (jana) jijini Dar es salaam mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Ninatubu Lema amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kuwaamini wahandisi wa ndani kutokana na kazi nzuri zinazofanyika na hatua kubwa iliyofikiwa katika utoaji wa huduma bora za ushauri na ujenzi tofauti na kipindi kilichopita.
Amesema katika kuimarisha na kuboresha huduma za ushauri na ujenzi nchini Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini kwa kushirikiana na wadau wengine wa taasisi za kihandisi pamoja na wale wa Jumuiya ya Kihandisi watakutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuoinyesha jamii kile ambacho wahandisi wa Kitanzania wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo nchini.
Ameeleza kuwa hivi sasa kuna wahandisi wengi wanaofanya shughuli za usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu nchini ikiwemo miradi ya barabara , gesi na shughuli za uchimbaji wa madini pia wapo wahandisi wa kitanzania wanaofanya kazi za ushauri katika mataifa mbalimbali ndani na ne ya bara la Afrika.
‘’Kwa upande wetu Tanzania wakati tunapata uhuru tulikua na wahandisi 2 na sasa wako zaidi ya elfu kumi ,jambo hili ni kubwa kwa sababu mchango wa wahandisi sasa tunauona katika kuleta maendeleo ya taifa maana bila ya kuwa na wahandisi vitu vyote tunavyoviona kama barabara, majengo, na miundombinu mbalimbali haviwezi kuwepo”
Prof. Lema amesema maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini yanalenga kuwatambua wahandisi na makampuni na mashirika ya Kihandisi yaliyotoa mchango mikubwa ya kihandisi katika maendeleo ya taifa na kuwahamasiha wahandisi wengine kufanya shughuli zao vizuri zaidi.
Ameongeza kuwa maadhimisho yataambatana na tuzo mbalimbali zenye lengo la kuwatia Moyo wanafunzi wahitimu kutoka vyuo vikuu na Taasisi za Uhandisi nchini pamoja na taasisi zitakazotia fora kwenye maonyesho ya ufundi pia kuwafanya vijana washawishike kusomea taaluma ya uhandisi.
Kwa upande wake msajili wa Bodi ya Usajili wa wahandisi Eng. Steven Mlote akizungumzia kuhusu ubora wa majengo yanayoendelea kujengwa kwa wingi jijini Dar es salaam amesema kuwa wamiliki wa majengo hayo wanao mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa majengo yao unazingatia viwango.
Amesema yeye kama msajili anawashauri wamiliki wa majengo kuhakikisha kuwa majengo yao yanayojengwa hivi sasa yanajengwa na wahandisi waliosajiliwa huku akitoa tahadhali kwa wale wanaokiuka kanuni zilizowekwa katika kusimamia ujenzi wa majengo nchini.
“Nawaomba wamiliki wote kuhakikisha kuwa pindi wanapoanza ujenzi wa majengo yao wahakikishe kuwa wanawatumia makandarasi waliosajiliwa, na mtu yeyote anayeruhusu jingo lake kujengwa na watu au kandarasi zisizosajiliwa anakiuka sheria na anastahili kushtakiwa” amebainisha Mlote.
Kwa upande wake Eng. Benedict. Mukama amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuyabaini majengo yote yanayojengwa nchini chini ya viwango na kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya makandarasi wanaohusika na ujenzi wa miradi hiyo huku akieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2011/2012 zaidi ya miradi 164 iliyokuwa inajengwa kinyume cha utaratibu bila kuzingatia viwango ikiwemo ya barabara imesimamishwa.
Aidha amesema maadhimisho haya ya siku ya wahandisi 2012 ambayo yanaadhimishwa nchini kwa mara ya 10 yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kuwa yanawawahusisha washiriki kutoka kutoka nchi za Maziwa Makuu,Afrika ya Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC).
Tuesday, February 28, 2012
LIST OF DELETED CONTRACTORS
Monday, February 27, 2012
Ardhi University Set to Survey Gas Pipeline Route
Asbestos ni hatari kwa afya: Je, Wanafunzi hawa wako salama?
Kwa sasa karibia kila nchi duniani imekwishapiga marufuku matumizi ya bidhaa hii kutokana na atahri za kiafya zinazosababbishwa na vipande vidogo vidogo vya bidhaa hii kuingia kwenye mwili wa binadamu kwa mfumo wa hewa na kuleta madhara.
Nchini Tanzania pia bidhaa hii ilikwisha kupigwa marufuku kutumika na kiwanda chake kilichokuwepo pembezoni mwa kiwanda cha cement Wazo Hill, Dar es Salaam, njia ya Bagamoyo kilishafunga uzalishaji wa bidhaa hii.
Wataalamu wanatuambia kuwa bidhaa ya asbestos ina madhara zaidi ukiwa unaitoa kwenye paa tofauti na ukiwa unaiweka/unaiezeka kama inavyoelezwa humu. Inaelezwa pia hata uchakavu wa bidhaa hii kutokaka na kukaa muda mrefu na kuathiriwa na hali ya hewa, bado madhara yatokanayo na bidhaa hii ni makubwa kwa afya ya mwanadamu endapo itatokea akavuta chembechembe ndogo kwa njia ya hewa.
Mamlaka inayoshughulika na mazingira nchini,NEMC imeweka utaratibu maalumu wa kutumia wataalamu katika kuteketeza mabaki ya bidhaa za asbestos ili zisiweze kuleta madhara kwa binadamu nchini.
Pichani wanaonekana wanafunzi nje ya darasa ambalo limeezekwa kwa kutumia bidhaa hii ya asbestos ambayo imepigwa marufuku kutumika nchini na sehemu nyingine duniani. Hii ni shule mpya ya Suye, ipo Jijini Arusha (shule ya Kata) na ndio imeanza wiki chache zilizopita. Jengo hili la darasa ni chumba ambacho hapo awali kilikuwa ni chumba cha kiwanda cha matofali. Kutokana na uhaba wa nafasi za watoto kuweza kusoma, Serikali ikaamua kuyabadilisha majengo hayo ili yapatikane madarasa kwa ajili ya kuwapokea wananfunzi hawa wa kidato cha kwanza. Sitaki kuamini wataalamu wa ujenzi walioshirikishwa hawakuona hatari ya kuwaweka watoto nadani ya mabati haya ambayo pasi na shaka yamekwishachakaa sana na uwezekano wa sumu kutoka ni mkubwa sana.
Hata hivyo, kitaalamu zipo namna za kuweza kuzuia madhara bila kuyaezua mabati haya. Ni zoezi ambalo linagharimu fedha kiasi. Lakini kwa hii shule, japo sio madarasa yote yana hii biidhaa, bado hakuna dalili za uwezekano kuwa kuna tahadhari yeyote imechukuliwa kudhibiti madhara ya sumu ya asbetos isiweze kuwadhuru wanafunzi hawa. Afya za watoto hawa ziko salama kiasi gani!?
Friday, February 24, 2012
Designer wetu wa leo..
Hii ni moja ya design iliyofanywa na vijana wa kitanzania. Ni mfano wa makazi bora kwa mwanadamu hasa katika ulimwengu huu wa sasa wa maendeleo ya kiteknolojia...
Mhusika wa kazi hii ni Masunga Matondo ambae ni Achitect/Designer na unaweza kutembelea ukurasa wake wa Facebook kwa kupitia kwa link hiyo ya jina lake moja kwa moja. Tupende kutumia vyakwetu na wataalamu wetu.
Blog hii itakuletea kazi nyingi za kijana huyu mwenye kipaji cha ubunifu wa kipekee.
Announcement: Contractors Training Course on 27th February 2012
The fees for the course is TShs 200,000/= per person for Registered Contractors.
Other cources for Contractors and other construction industry practitioners under SSTP Programme for 2012 are scheduled to happen as follows..
Kigoma 26th-30th March 2012
Arusha 16th-20th April 2012
Iringa 30th July-3rd August 2012
Dar es Salaam 27th-28th September 2012
Lindi 24th-28th September 2012.
For more details please visit the Contractors Registration Board's official website
Friday, February 10, 2012
APPOINTMENT OF A REGISTRAR - AQRB
Tuesday, February 7, 2012
Maisha marefu katika nyumba bora...
Binadamau ni mmoja kati ya viumbe hai ambae hupenda kukaa mahali akajisikia raha. Afya ya binadamu huyu hutegemeana na mazingira anayoishi hususani mahali anapolala. Nyumba bora kwa viwango stahili huakisi afya bora kwa mtumiaji!
Nyumba kama hii inayoonekana pichani haiwezi kutoa uhakika wa afya ya aneishi kwa msingi kwamba vumbi pekee linatosha kusababisha athari za kiafya kwa watumiaji! Nyumba kama hizi yafaa sasa zibaki kama historia ya kizazi chetu kilipotoka, tuanze kuwazia nyumba bora kwa nchi nzimaWakulima na wafugaji vijijini ndio wanaonekana kuishi kwenye makazi duni zaidi kwasababu ya tabia yao ya kuhamahama.









