Header Ads

Header Ads

Asbestos ni hatari kwa afya: Je, Wanafunzi hawa wako salama?

Asbestos ilitumika zaidi kama bidhaa ya ujenzi wa majumba kati ya miaka ya 1950 na 1970. Bidhaa hii ilipendwa zaidi kutokana na uwezo wake wa kutunza hali ya joto au ubaridi.
Kwa sasa karibia kila nchi duniani imekwishapiga marufuku matumizi ya bidhaa hii kutokana na atahri za kiafya zinazosababbishwa na vipande vidogo vidogo vya bidhaa hii kuingia kwenye mwili wa binadamu kwa mfumo wa hewa na kuleta madhara.

Nchini Tanzania pia bidhaa hii ilikwisha kupigwa marufuku kutumika na kiwanda chake kilichokuwepo pembezoni mwa kiwanda cha cement Wazo Hill, Dar es Salaam, njia ya Bagamoyo kilishafunga uzalishaji wa bidhaa hii.

Wataalamu wanatuambia kuwa bidhaa ya asbestos ina madhara zaidi ukiwa unaitoa kwenye paa tofauti na ukiwa unaiweka/unaiezeka kama inavyoelezwa humu. Inaelezwa pia hata uchakavu wa bidhaa hii kutokaka na kukaa muda mrefu na kuathiriwa na hali ya hewa, bado madhara yatokanayo na bidhaa hii ni makubwa kwa afya ya mwanadamu endapo itatokea akavuta chembechembe ndogo kwa njia ya hewa.

Mamlaka inayoshughulika na mazingira nchini,NEMC imeweka utaratibu maalumu wa kutumia wataalamu katika kuteketeza mabaki ya bidhaa za asbestos ili zisiweze kuleta madhara kwa binadamu nchini.

Pichani wanaonekana wanafunzi nje ya darasa ambalo limeezekwa kwa kutumia bidhaa hii ya asbestos ambayo imepigwa marufuku kutumika nchini na sehemu nyingine duniani. Hii ni shule mpya ya Suye, ipo Jijini Arusha (shule ya Kata) na ndio imeanza wiki chache zilizopita. Jengo hili la darasa ni chumba ambacho hapo awali kilikuwa ni chumba cha kiwanda cha matofali. Kutokana na uhaba wa nafasi za watoto kuweza kusoma, Serikali ikaamua kuyabadilisha majengo hayo ili yapatikane madarasa kwa ajili ya kuwapokea wananfunzi hawa wa kidato cha kwanza. Sitaki kuamini wataalamu wa ujenzi walioshirikishwa hawakuona hatari ya kuwaweka watoto nadani ya mabati haya ambayo pasi na shaka yamekwishachakaa sana na uwezekano wa sumu kutoka ni mkubwa sana.

Hata hivyo, kitaalamu zipo namna za kuweza kuzuia madhara bila kuyaezua mabati haya. Ni zoezi ambalo linagharimu fedha kiasi. Lakini kwa hii shule, japo sio madarasa yote yana hii biidhaa, bado hakuna dalili za uwezekano kuwa kuna tahadhari yeyote imechukuliwa kudhibiti madhara ya sumu ya asbetos isiweze kuwadhuru wanafunzi hawa. Afya za watoto hawa ziko salama kiasi gani!?

No comments: