• Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?

    Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.

  • Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?

    Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.

  • Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?

    Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Saturday, January 19, 2013

Umeshawahi kufikiria kuwa na sakafu ya mbao ndani ya nyumba yako?

DSCN7253Sakafu ya mbao, kitaalamu inaitwa “Parquet Flooring”. Sakafu hii kama picha inavyoonesha imeunganishwa na tiles zenye rangi inayofanania nazo
DSCN7263Hizi ni stepu za ngazi ambazo zimewekewa mbano ngumu badala ya tiles ama bidhaa nyingineyo. Iking’arishwa na varnish/polish hupendeza sana!
DSCN7275
DSCN7296Sakafu hii ni ya mbao tupu kabla ya kung’arishwa

External Pavings kwa kutumia mawe ya mtoni

DSCN7304Leo Blog yako ya ujenzi inakuletea teknolojia mpya ya kutengeneza madhari ya kuzunguka nyumba na kwa kutumia mawe madogomadogo yanyopatikana mtoni.

Kama picha inavyoonesha mawe haya madogo hupangwa kwa kuunganishwa karibu juu ya surface ngumu iliyoandaliwa maalumu, na baadae kukaziwa na mchanganyiko wa sementi na mchanga kwenye maunganiko. Haya hutumiak kama mbadala wa paving blocks, slabs, tiles ama screeding ya kawaida.
DSCN7249