• Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?

    Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.

  • Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?

    Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.

  • Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?

    Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Saturday, December 15, 2012

JK AZINDUA NYUMBA ZA BEI NAFUU ZA NHC KIBADA, KIGAMBONI,DAR

Rais Jakaya Kikwete (alivaa koti la rangi ya maziwa) akikagua moja kati nyumba 290 za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Kibada, Kigamboni Dar es Salaam Desemba 13,2012. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

JK akisalimiana na wafanyakazi wa NHC alipowasili kuzindua nyumba hizo

                                              Kikundi cha hamasa kikitumbuiza

JK akitoa maelezo kwa Mchechu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck ole Medeye wakati wa uzinduzi wa nyumba hizo.

                                    JK akiwa na baadhi ya maofisa wa NHC

Baadhi ya nyumba zilizozinduliwa  na Rais Kikwete











IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AKABIDHI NYUMBA MPYA 35 ZA WALIOATHIRIKA NA MILIPUKO YA MABOMU YA GONGO LA MBOTO JANA JIJINI DAR ES SALAAM



Picha juu ni Baadhi ya  nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto  katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama zinavyoonekqana  leo Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete

kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa  kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto  katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012

Bila kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya serikali ya kujenga  nyumba mpya 35 kwa ajili ya  waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume, amejengewa nyumba ya vyumba vitano pamoja na fremu ya duka.Picha na IKULU







Saturday, December 8, 2012

MAONESHO YA NYUMBA YAANZA DAR

 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya Nyumba yaliyoandaliwa na Kampuni ya Tanzania Home Export
kwenye viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam kwa siku tatu kuanzia leo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Matukio wa kampuni hiyo,Zeno Ngowi na Rhoda Furaha.

Baadhi nyumba za kuuzwa zinazojengwa na Kampuni ya Sea Breeze eneo la Jangwani, Mbezi Beach Dar es Salaam.

                                           Wananchi wakiangalia nyumba hizo


                                         Moja ya mabanda yaliyopo kwenye maonesho hayo

DC Rugimbana akisalimiana na  Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa  Benki ya Azania, Othman Jabrie alipotembelea banda hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akitembelea banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Rugimbana akizungumza na Mkuu wa Fedha Mwandamizi wa TMRC, Oswald Urassa. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO – RICHARD MWAIKENDA)