• Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?

    Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.

  • Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?

    Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.

  • Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?

    Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Sunday, April 24, 2016

A simple 3 bedrooms residential house 3D model

Muonekano wa mbele

Mounekano wa upande wa ubavuni kulia

Muonekano wa nyuma na baraza ya jikoni/uwani

Upande wa ubavuni kushoto

Mfano wa ubunifu wa jengo la makazi hatua za awali..

Picha hizi zinaonesha mfano wa muonekano wa nje (in 3D view) wa jengo la makazi lililobuniwa kabla ya kujengwa.

Wataalamu wa ubunifu majengo (Architects) hubuni muundo wa jengo mfano kama huu na kisha kusimamia ujenzi wake ili kupata jengo halisi kama lilivyobuniwa.

Katika muonekano wa picha hizi, bado umaridadi wa nje na mazingira na muonekano halisi wa jinsi jengo litakavyokuwa haujakamilika. Lakini mpaka hatua hii tayari unaweza kuwa na michoro (floor plan) na kufanya ujenzi. Hapa bado kuna  hatua zaidi mchoro unapitishwa kwenye program maalumu na kuongeza uhalisia.

Kwa mahitaji binasi ya huduma za ushauri na ubunifu wa jengo lako unalowazia, pamoja na  makadirio ya gharama zake  unaweza kuwasiliana nasi.

Karibu!



SeriaJr

Sampuli mbili tofauti za "Paving Blocks" na gharama zake


Aina ya kwanza, umbo duara.. Rangi  tofauti

Aina ya pili umbo mraba uliobonyea pande zote

Picha hii inaonesha sampuli mbili zimechanganywa pamoja kupata aina moja ya madoido
******

Kuna aina na muundo tofauti tofauti wa vitofali vya kusakafia mandhari ya nje au eneo la maegesho ya gari au njia ya kupita kuelekea kwenye jengo lako, aidha la kuishi, karakana au kuhifadhia bidhaa. Na hata bustanini.

Mpangilio wa vitofali hivyo huweza kuleta unaridadi mwingine tofauti. Picha hizi zinaonesha aina mbili za muundo wa vitofali hivyo ambavyo ukivichanganya pamoja unapata umaridadi fulani.

Kwa mkazi wa Dar es Salaam hasa maeneo ya Kinondoni na Kibamba nimekusogezea mdau anayezalisha hizi bidhaa.

Kwa wenye uhitaji wa "paving blocks" katika umaridadi tofauti, bei ya soko ni sh 15,000 hadi 18,000 kwa eneo la "square metre" moja zinaingia vipande 50.

Wasiliana na mdau huyu kwa nambari 0786808707!


Mhandisi ni nani hasa kwenye ujenzi? Ipi tofauti ya Mhandisi na Mkandarasi!?


Ubunifu wa nondo na mpangilio wake, ubora wa zege na aina ya msingi wa jengo ni moja kati ya kazi wa mhandisi. Picha hii inaonesha sehemu ya msingi wa nyummba ya ghorofa moja

Kumekuwapo na mkanganyiko miongoni mwetu kuhusiana na wataalamu wa ujenzi wajuikanao kama wahandisi (Engineers) na wanataaluma wengine na hasa mkandarasi. Wapo wataalamu wengi wa ujenzi lakini kuna makosa yanafanyika na kuwafananisha watu wote kama wahandisi.
Wahandisi/(Civil and Structural Engineers)
Kawaida katika taratibu za ukamilifu wa mradi wa ujenzi kuanzia hatua ya awali kabisa, baada ya Mbunifu majengo kumaliza kazi ya kuandaa michoro yake mhadisi ndiye mtaalamu wa pili kuweka utaalamu wake.

Mara nyingi kumekuwapo na mchanganyo wa uhandisi na ukandarasi. Kuweka hili sawa kupitia blogu hii, ifahamike kuwa mhandisi ni mtaalamu mbunifu wa uimara wa jengo na mkandarasi ni mjenzi wa jengo akifanyika kazi vilivyobuniwa na wahandisi na wabunifu majengo.

Mkandarasi anaweza kuwa aidha mtu binafsi au kampuni iliyosajiliwa kufanya kazi ya ujenzi kwa kiwango fulani.


Sasa huyu anayejulikana kama Structural Engineer ndiye Mhandisi hasa na huwajibika kwa uhandisi wa ubora na uimara wa jengo kwa kufanya mahesabu ya uimara (strength), uzito, nguvu na namna vitakavyokabiliana bila kuleta madhara kwenye jengo linalotarajiwa kujengwa.


Moja ya kazi za kinadisi kwenye nyumba ya kawaida
Ni jukumu la mhandisi huyu kuandaa michoro ya uimara wa jengo kwa maana ya namna nondo na zege na hata vyuma vingine vitakavyokuwa na ukubwa wake kwa maeneo kama nguzo (column), msingi (foundation) bimu (beams), kuta, ngazi za ghorofa na slabu (slabs) kwa upande wa majumba. Halikadhalika huandaa michoro kwa ajili ya madaraja, nguzo kubwa, mabwawa n.k. 


Wakati wa ujenzi anakagua pia ubora wa bidhaa (materials) zinazotumika na namna nondo na zege zinavyotengenezwa kama vinafikia ubora unaotakiwa kama alivyobuni kimahesabu.

Inapotokea jengo limeanguka kwasababu zisizotokana na nguvu za asili kama mtetemeko ya ardhi na milipuko ya bomu kwa mfano, mhandisi ndiye hupewa majukumu ya kuchunguza sababu za kihandisi zilizopelekea hitilafu iliyosabababisha jengo kuanguka kama iivyotokea maeneo ya Kisutu Jijini Dar es Salaam miaka michache iliyopita. 

Tuesday, April 19, 2016

RAIS MAGUFULI AFUNGUA DARAJA LA KIGAMBONI RASMI, LIMEGHARIMU SH BIL 214.6

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.PICHA NA IKULU

Saturday, April 16, 2016

RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLAI OVA) ENEO LA TAZARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua  jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua ramani ya mradi wa barabara ya juu eneo la Tazara kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi huo Tazara Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea maelekezo kuhusu mradi wa barabara za juu eneo la Tazara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale katika ufunguzi rasmi wa mradi huo Jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018.

Sherehe ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida.

Barabara hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.

Barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha upotevu wa shilingi Bilioni 411.55

Rais Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara  ya njia sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano, ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi hospitali ya Agha Khan.

Juhudi nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe.

Aidha, Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika.

Dkt. Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Aprili, 2016

Wednesday, April 6, 2016

NGAWAIYA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJENGA GHOROFA BILA KUTUMIA WAKANDARASI WALIOSAJILIWA


Mfanyabiashara na mwansiasa wa muda mrefu Bw Thomas Ngawaiya, aambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa madai ya kufanya shughuli za ujenzi wa ghorofa kinyume cha sheria namba 17 kifungu 22(4) ya ukandarasi ya mwaka 1997
Akisoma kesi hiyo namba 322, Saddy Kambona, Wakili wa Serikali mbele ya Helen Liwa, Hakimu Mkazi amesema kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 24 Machi, 2015 katia Mtaa wa Dosi na Wazani, Magomeni Dar es Salaam.
Kambona amesema, Ngawaiya alitumia wajenzi wasio wakandarasi waliosajiliwa na bodi ya wakandarasi nchini kujenga jingo la hoteli lenye thamani ya zaidi ya Sh. 500 milioni. Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 20 Aprili mwaka huu.

SERIKALI YAZUIA MAKAMPUNI YA NJE KUANDAA WA MASTER PLAN NCHINI.



 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi (Mb), akitoa maagizo kadhaa wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kushoto kwake ni Mwenyekiti  mpya wa bodi hiyo; Prof. Wilbard Kombe na kulia kwake ni Mwenyekiti mstaafu, John Lubuva.

Mwenyekiti  mpya wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji; Prof. Wilbard Kombe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji; Bwn.John Lubuva akitoa taarifa fupi ya bodi hiyo, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) ametangaza rasmi mwisho wa kutumia Makampuni ya nje katika kazi za kuandaa Master plan. Mhe. Lukuvi aliyasema hayo wakati akizindua rasmi bodi ya wataalam wa Mipango Miji Wizarani hapo.

Lukuvi amesema nchini kuna wataalam wengi na wenye elimu ya kutosha kwa ajili ya kufanya kazi ya kuandaa Master plan, lakini kumekuwa na taratibu za kutafuta wataalam hao kutoka nchi za nje. Alisema; “ Ninaagiza kuwa sasa ni mwisho wa kuajiri makampuni ya nje, kazi za master plan zisimamiwe na bodi hii kwa kutumia makampuni ya humu humu nchini”.

Ameendelea kusema kuwa’ “ Sasa Bodi ya Wataalam wa Mipango Miji itapaswa kuhusika kikamilifu katika zoezi la Upangaji, upimaji na umilikishwaji wa ardhi kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuhakikisha kuwa suala la uwazi katika upangaji miji linazingatiwa”.

Vile vile alisema kuwa bodi itapaswa kuhakikisha Wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika kulipia gharama kadhaa kwa huduma wanazopatiwa na bodi. Mhe. Lukuvi alisema kuwa bodi hiyo haitaitwa tena bodi ya Mipango Miji, bali itajulikana kama bodi ya Mipango Miji na Vijiji.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa bodi; Prof. Wilbard Kombe alimuomba Lukuvi kuzitaka Halmashauri kushiriki vyema katika kutoa elimu kwa umma kwa kuwa na utayari wa kutoa taarifa zinazopaswa kuwasilishwa kwa Wananchi kwa wakati ili waweze kuelewa vyema kuhusu mipango inayohusu maeneo yao.

WAZIRI PROF. MBARAWA AKAGUA DARAJA LA RUSUMO NA VITUO VYA PAMOJA VYA FORODHA KABLA YA UFUNGUZI.

LUS5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale wakati akikagua Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
LUS1
Muonekano wa barabara ya Nyakahura-Rusumo inayounganisha Tanzania na Rwanda kupitia Daraja la Rusumo wilayani Ngara.

LUS2
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wa pili kulia akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia), alipotembelea ofisi hizo katika Kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Border Post) upande wa Tanzania kilichopo Rusumo wilayani Ngara, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga.
LUS3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (mwenye kofia) wakati akikagua maandalizi ya ufunguzi wa Daraja la Rusumo na Vituo vya pamoja vya forodha (One Stop Border Post) wilayani Ngara.
LUS4
Muonekano wa Daraja la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda, kushoto ni daraja la zamani lenye rangi ya njano na kulia ni daraja jipya.
LUS6
Meneja wa Kituo cha pamoja cha forodha(One Stop Border Post), katika mpaka wa Tanzania na Rwanda upande wa Rwanda Bw. Moses Kalisa akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Thursday, March 3, 2016

RAIS DKT.MAGUFULI NA RAIS UHURU KENYATTA WAWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA ARUSHA-HOLILI/TAVETA-VOI YA KM 234.3 Na: SeriaJr TW on Thursday, March 03, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya sherehe za unzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi wa Arusha hawapo pichani kabla ya ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwaongoza Marais wa Kenya, Uganda, Makamu wa Rais wa Sudani Kusini pamoja na Burundi kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimwagilia mti maji pamoja na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya sherehe za uzinduzi wa barabara hiyo kukamilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(Nairobi) Gabriel Negata mara baada ya uzinduzi wa barabara hiyo ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Tengeru nje kidogo ya Jiji la Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda, Yoweri Meseveni na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukipigwa kabla ya uzinduzi wa barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU

Monday, January 11, 2016

Ukifuata Hatua Hizi Huwezi Kubomolewa Nyumba Yako


Wakati baadhi ya wakazi wa mabondeni wakisaka hifadhi baada ya nyumba zao kubomolewa, wataalamu wa ardhi na maendeleo ya makazi wametoa njia za kumaliza adha hiyo zikiwamo Serikali kurahisisha mfumo wa urasimishaji ardhi na wananchi kufuata taratibu stahiki za ujenzi ili nyumba zao zisibomolewe.

Wataalamu hayo walisema kwa nyakati tofauti kuwa tatizo kubwa lililosababisha dhahama hiyo ni ukosefu wa elimu ya ardhi na mipango miji miongoni mwa wananchi na Serikali kulegalega katika kusimamia mambo hayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya maendeleo ya makazi ya Space and Development, Renny Chiwa alisema uelewa mdogo katika matumizi ya ardhi na mipango miji umewafanya Watanzania wengi kujenga kiholela katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya wazi na mabondeni.

“Kwa sasa mtu akiona ardhi tu anataka kujisitiri bila kuulizia na kufuata taratibu. Serikali na wadau wanatakiwa kutoa elimu ya kutosha juu ya umiliki wa ardhi na matumizi yake,” alisema.

Chiwa aliwataka wataalamu wa wizara ya ardhi washirikiane na taasisi zinazotoa huduma muhimu kwa jamii kama Shirika la Umeme (Tanesco) na Kampuni ya huduma ya Majisafi (Dawasco) katika kudhibiti uendelezaji wa maeneo hatarishi na wazi.

Alisema Tanesco na Dawasco wamechangia kwa kiasi kikubwa kuvutia watu kujenga katika maeneo yasiyotakiwa kwa kuwa waliunganisha huduma kwa wakazi hao wakati wakijua bayana hapafai.

“Yale maeneo ya mabondeni yote yalikuwa na umeme na maji ya Dawasco. Wao wanawaza kuongeza wateja na fedha tu lakini kwa nchi kama Kenya taasisi hizo zinashirikiana na wataalamu wa ardhi kuzuia uendelezaji huo holela,” alisema.

Njia nyingine ya kukomesha ujenzi holela, Chiwa alitaja kuwa ni Serikali kuyabaini maeneo yote ya wazi, kuyawekea alama na kuyaendeleza ili yasivutie watu kuyavamia.

Alisema Serikali inaweza kutafuta wawekezaji wa sekta binafsi ambao wataendeleza kwa kutoa huduma za burudani katika maeneo hayo ya wazi kuliko kuyaacha bila kuyaendeleza.

Ili kumaliza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa, Chiwa alishauri kuchochea ukuaji wa sekta binafsi katika uendelezaji wa ardhi na makazi kwa kuwa Serikali ina watumishi wachache ambao hawawezi kumudu mahitaji ya sasa ya upimaji na uendelezaji ardhi.

Chiwa alipendekeza ramani za mipango miji zipelekwe ngazi za kata badala ya kukaa wizarani na watumishi wa kada za chini za ardhi wenye elimu ya vyeti na stashahada wapelekwe kila kata kutoa huduma hizo kwa ushirikiano na viongozi wa Serikali za mitaa.

“Hii itafanya watu wengi wapime ardhi zao kwa hiari kwa kuwa hakuna urasimu na hatimaye wataacha kuvamia ardhi na tabia ya kujenga kiholela bila kufuata mipango miji,” alisema Chiwa.

Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Ilala, Alfred Mbyopyo alisema wananchi wanaweza kuepuka kujenga kiholela kwa kununua viwanja vilivyopimwa au kurasimisha maeneo yao waliyoyanunua kienyeji.

Alisema kwa wale walionunua viwanja vya halmashauri za wilaya vikiwa vimepimwa na kupatiwa hati wanatakiwa kuandaa michoro yao kupitia kwa msanifu majengo yoyote na kuipeleka halmashauri kupata vibali vya kujenga ili kuepusha matatizo.

Mbyopyo alisema kwa wale wanaonunua mashamba au maeneo kienyeji wanaweza kurasimisha na kupata hati za umiliki sawa na walionunua viwanja vikiwa vimepimwa wakianzia na ngazi za Serikali za Mitaa.

“Ukishauziwa eneo lako kama ni miguu 20 kwa 20 kama ambavyo wengi hupima unatakiwa uwatafute maofisa ardhi wa halmashauri au wataalamu binafsi kupima. Ningeshauri wafanye upimaji kwa makundi ili kuokoa gharama,” alisema.

Kwa wapimaji binafsi alisema, watapata vibali vya kupima eneo husika kutoka kwa halmashauri ya Manispaa kuruhusu upimaji wa maeneo husika.

Baada ya kupimiwa na kupata vipimo vya ardhi zao na kubainishiwa havina matatizo yoyote, wanapaswa waende halmashauri husika kwa ajili ya kuhakikisha michoro ya eneo na matumizi yake.

Alisema wapimaji hao watachukua nyaraka hizo na kwenda nazo Wizara ya Ardhi na kupatiwa namba ya kiwanja kupitia idara ya upimaji.

Baada ya kupatiwa namba mwombaji au mtaalamu wake watarudi halmshauri kwa ajili ya kibali cha umiliki baada ya ofisa ardhi na mipangomiji kujiridhisha na mpango wa hati utaandaliwa tayari kupelekwa kwa Kamishna wa Ardhi wa Kanda kwa ajili ya usajili na hati ambayo hutolewa na msajili wa ardhi.

Mbyopyo alisema suala la hati halihusishi kundi kwa waliopima kwa pamoja, bali ni la mtu binafsi kwa kuwa kuna gharama zake, hivyo ni bora wataalamu waliohusika kupima wakatumika kufanikisha upatikanaji wa hati hizo.

Kama ilivyo kwa wenye viwanja vilivyopimwa, Mbyopyo alisema wamiliki wa maeneo ya kienyeji yaliyopatiwa hati na Serikali watafuata taratibu za kupeleka michoro na kuruhusisha kujenga.

Lukuvi aja na mkakati mpya
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema jana kuwa wananchi wanapaswa kuthibitisha matumizi ya ardhi husika kabla kununua ili kuzuia hasara.

Alisema kuna baadhi ya maeneo yanaonekana ni mapori ila ni sehemu za wazi au kwa ajili ya huduma hivyo uthibitisho kwa Serikali za Mitaa na Halmashauri ni nguzo ya kuzuia utapeli na kadhia ya kubomolewa.

“Watu wengi wanakurupuka tu kupata viwanja na kujenga. Wengine wanaanza kujenga halafu ndiyo wanaanza kutafuta hati, baadaye wanakuta eneo lile ni la wazi au la huduma za shule na kutakiwa kubomoa,” alisema Lukuvi.

“Hakikisha unapata kibali cha kujenga kwa sababu ukipata kibali unampa kazi mtoa kibali kufuatilia undani wa eneo lako na iwapo akikuruhusu ujenge halafu mambo yabadilike, watalazimika wakulipe fidia.”

Lukuvi alisema ili kurahisisha mchakato wa upimaji ardhi, wizara inazidi kusajili kampuni nyingi binafsi za kupima ardhi kwa kuwa Serikali haina wataalamu wengi wa kupima.

Mbali na kuongeza wapimaji, alisema ataanza kuzidhibiti bei kubwa za uuzaji wa viwanja zinazotumika sasa na halmashauri nchini na kusababisha wananchi wengi kukosa viwanja.

Alisema halmashauri zimegeuza upimaji na uuzaji wa viwanja kama chanzo kikubwa cha mapato huku zikiwanyonya wamiliki wa mashamba ambayo huchukuliwa kwa kuwapa fidia kidogo.

“Nataka baada ya kupima eneo, wanavyoleta michoro ya eneo nataka walete na mapendekezo ya bei zao tuzione na kutoa bei elekezi. “Wananchi wengi wenyeji wameshindwa kununua viwanja kwa sababu ya bei kubwa. Wao hulipwa fedha kidogo za fidia na kuuziwa kwa gharama za mara 500 au 1,000, safari hii hatutakubali,” alisema Lukuvi.

Alisema Serikali imeagiza vifaa vingi vya kupimia ardhi vitakavyowekwa kwenye ofisi tisa za kanda na halmshauri zote zisizokuwa na vifaa zitakuwa zinaenda kuchukua pale kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Katika mipango hiyo mipya, Lukuvi alisema shughuli za uthamini ardhi na majengo, utoaji wa vibali vya mikopo kupitia ardhi, usajili na utoaji wa hati zinafanyika ofisi za kanda na kwamba hakuna haja ya mwananchi kwenda wizarani.

“Kamishna Mkuu wa Ardhi sasa hatatia sahihi mambo yote yafanyike huko. Nataka muda wa chini kupima hadi kuchukua hati uwe mwezi mmoja na kipimo cha juu miezi mitatu. Mwananchi yoyote atakayepata hati baada ya miezi mitatu anijulishe niwashughulikie maofisa wa halmashauri hiyo,” alisema Lukuvi.

CHANZO: MWANANCHI, JANUARI 11, 2016
www.mwananchi.co.tz/habari/ukizifuata-hatua-hizi-huwezi-kubomolewa/-1597578/3028712/-p9ilsb/-/index.html