-
Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?
Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.
-
Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?
Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.
-
Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?
Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.
Sunday, April 24, 2016
A simple 3 bedrooms residential house 3D model
Mfano wa ubunifu wa jengo la makazi hatua za awali..
Picha hizi zinaonesha mfano wa muonekano wa nje (in 3D view) wa jengo la makazi lililobuniwa kabla ya kujengwa.
Wataalamu wa ubunifu majengo (Architects) hubuni muundo wa jengo mfano kama huu na kisha kusimamia ujenzi wake ili kupata jengo halisi kama lilivyobuniwa.
Katika muonekano wa picha hizi, bado umaridadi wa nje na mazingira na muonekano halisi wa jinsi jengo litakavyokuwa haujakamilika. Lakini mpaka hatua hii tayari unaweza kuwa na michoro (floor plan) na kufanya ujenzi. Hapa bado kuna hatua zaidi mchoro unapitishwa kwenye program maalumu na kuongeza uhalisia.
Kwa mahitaji binasi ya huduma za ushauri na ubunifu wa jengo lako unalowazia, pamoja na makadirio ya gharama zake unaweza kuwasiliana nasi.
Karibu!
SeriaJr
Sampuli mbili tofauti za "Paving Blocks" na gharama zake
Aina ya kwanza, umbo duara.. Rangi tofauti
Aina ya pili umbo mraba uliobonyea pande zote
Picha hii inaonesha sampuli mbili zimechanganywa pamoja kupata aina moja ya madoido
******
Kuna aina na muundo tofauti tofauti wa vitofali vya kusakafia mandhari ya nje au eneo la maegesho ya gari au njia ya kupita kuelekea kwenye jengo lako, aidha la kuishi, karakana au kuhifadhia bidhaa. Na hata bustanini.
Mpangilio wa vitofali hivyo huweza kuleta unaridadi mwingine tofauti. Picha hizi zinaonesha aina mbili za muundo wa vitofali hivyo ambavyo ukivichanganya pamoja unapata umaridadi fulani.
Kwa mkazi wa Dar es Salaam hasa maeneo ya Kinondoni na Kibamba nimekusogezea mdau anayezalisha hizi bidhaa.
Kwa wenye uhitaji wa "paving blocks" katika umaridadi tofauti, bei ya soko ni sh 15,000 hadi 18,000 kwa eneo la "square metre" moja zinaingia vipande 50.
Wasiliana na mdau huyu kwa nambari 0786808707!
Mhandisi ni nani hasa kwenye ujenzi? Ipi tofauti ya Mhandisi na Mkandarasi!?
Ubunifu wa nondo na mpangilio wake, ubora wa zege na aina ya msingi wa jengo ni moja kati ya kazi wa mhandisi. Picha hii inaonesha sehemu ya msingi wa nyummba ya ghorofa moja |
Kumekuwapo na mkanganyiko miongoni mwetu kuhusiana na wataalamu wa ujenzi wajuikanao kama wahandisi (Engineers) na wanataaluma wengine na hasa mkandarasi. Wapo wataalamu wengi wa ujenzi lakini kuna makosa yanafanyika na kuwafananisha watu wote kama wahandisi.
Wahandisi/(Civil and Structural Engineers)
Kawaida katika taratibu za ukamilifu wa mradi wa ujenzi kuanzia hatua ya awali kabisa, baada ya Mbunifu majengo kumaliza kazi ya kuandaa michoro yake mhadisi ndiye mtaalamu wa pili kuweka utaalamu wake.
Mara nyingi kumekuwapo na mchanganyo wa uhandisi na ukandarasi. Kuweka hili sawa kupitia blogu hii, ifahamike kuwa mhandisi ni mtaalamu mbunifu wa uimara wa jengo na mkandarasi ni mjenzi wa jengo akifanyika kazi vilivyobuniwa na wahandisi na wabunifu majengo.
Mkandarasi anaweza kuwa aidha mtu binafsi au kampuni iliyosajiliwa kufanya kazi ya ujenzi kwa kiwango fulani.
Sasa huyu anayejulikana kama Structural Engineer ndiye Mhandisi hasa na huwajibika kwa uhandisi wa ubora na uimara wa jengo kwa kufanya mahesabu ya uimara (strength), uzito, nguvu na namna vitakavyokabiliana bila kuleta madhara kwenye jengo linalotarajiwa kujengwa.
Moja ya kazi za kinadisi kwenye nyumba ya kawaida |
Wakati wa ujenzi anakagua pia ubora wa bidhaa (materials) zinazotumika na namna nondo na zege zinavyotengenezwa kama vinafikia ubora unaotakiwa kama alivyobuni kimahesabu.
Inapotokea jengo limeanguka kwasababu zisizotokana na nguvu za asili kama mtetemeko ya ardhi na milipuko ya bomu kwa mfano, mhandisi ndiye hupewa majukumu ya kuchunguza sababu za kihandisi zilizopelekea hitilafu iliyosabababisha jengo kuanguka kama iivyotokea maeneo ya Kisutu Jijini Dar es Salaam miaka michache iliyopita.
Tuesday, April 19, 2016
RAIS MAGUFULI AFUNGUA DARAJA LA KIGAMBONI RASMI, LIMEGHARIMU SH BIL 214.6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.PICHA NA IKULU

Saturday, April 16, 2016
RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLAI OVA) ENEO LA TAZARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.

Wednesday, April 6, 2016
NGAWAIYA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJENGA GHOROFA BILA KUTUMIA WAKANDARASI WALIOSAJILIWA
SERIKALI YAZUIA MAKAMPUNI YA NJE KUANDAA WA MASTER PLAN NCHINI.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi (Mb), akitoa maagizo kadhaa wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo; Prof. Wilbard Kombe na kulia kwake ni Mwenyekiti mstaafu, John Lubuva.
Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji; Prof. Wilbard Kombe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.