• Unataka Kujenga Ukuta Imara wa Nyumba Yako Utakaodumu Muda Mrefu?

    Ukuta wa nyumba ni sehemu muhimu na ya kudumu katika jengo lolote. Huweka uimara wa jengo na kudhibiti joto la nje na la ndani sambamba na kuweka usiri wa vitu vilivyomo ndani ya jingo. Hutoa ulinzi na kuweka usalma dhidi ya matukio ya hatari na wizi kwa vitu ama watu waliomo ndani.

  • Tunakosa nini Tusipotumia Wataalamu katika Ujenzi Wetu?

    Kushirikisha wataalamu kunatoa fursa ya kujua mbinu mpya na bora za ujenzi, kufaahamu vifaa vya ujenzi na sifa zake, kujua namna ya kupata gharama nafuu za ujenzi na usanifu majengo kuendana na ndoto yako binafsi.

  • Unafahamu Nini Ukinunua Simenti Imeandikwa 32.5N au 42.5N?

    Kuna madaraja matatu ya ubora/uimara wa simenti/saruji ambayo ni uimara wa chini 32.5, uimara bora zaidi ya ule wa chini 42.5 na uimara wa juu zaidi 52.5. Saruji ya gredi 52.5 bado haijaanza kuzalishwa kwa soko la Tanzania. Hii ni kusema kwamba tuna gredi ya 32.5 na 42.5 tu.Simenti ya daraja la chini la ubora 32.5 inafaa zaidi kwa matumizi ya plaster na kazi ndogo ndogo, na ile ya daraja la juu zaidi yani 42.5 inafaa zaidi kwa kazi za zege kama nguzo, bimu, slabu, madaraja n.k kutokana na uimara wake kuwa mkubwa zaidi.

Wednesday, September 5, 2012

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AZINDUA UJENZI WA JENGO KUU LA ELIMU HURIA NA MASAFA

Picha ya pamoja, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa pamoja na Mama Maria Nyerere aliyekuwepo katika uzinduzi huo.

Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa kama linavyoonekana ambalo ujenzi wake umezinduliwa leo 5/9/2012 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Kawambwa



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk.Kawambwa akifurahi baada ya kuzindua ujenzi wa Jengo kuu la Elimu Huria na Masafa leo huku Mama Maria Nyerere akimpongeza.

Mama Maria Nyerere,Mhe.Dk.Kawambwa wakifurahia jambo na wageni wengine baada ya uzinduzi  wa Jengo 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Prof.Tolly Mbwette akitoa maelezo ya awali kuhusiana na ujenzi wa Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa kwa Wageni waalikwa katika uzinduzi waliokuja kushuhudia Uzinduzi huo leo 5/9/2012 katika Ofisi za Muda za Chuo Kinondoni,Dar es Salaam.
SOURCE: RUNDUGAI BLOG








ROOF CONSTRUCTION FOR RESIDENTIAL HOUSES

DSCN5202Kenji (truses) zikiwa zimeshikizwa kwenye bimu ya zege (reiforced concrete beam) kutengeneza paa la nyumba mtindo wa (pitch) kama linavyoonekana kwa kutokea ndani. Bolt na nati ndizo zimetumika kushikilia bimu zikikazwa kwa kucomewa (welding). Tie beam wametumia mbao mbili kwa uimara zaidi. Kwa kawaida kenji linaweza kuwa la chuma au mbao kutegemeana na uimara unaohitajika. Mbao za kenji zina ukubwa wa 150x50mm.

DSCN5230

Mbao ulalo kwa saizi ya unene wa 50x50mm zimewekwa kwa upana unaofanana. kwa kitaalamu mbao hizi huitwa purlins.

DSCN5209

Vigae hupangwa kimoja kimoja kwa kufuata purlins zilivyojipanga

DSCN5201

Monday, September 3, 2012

WAHANDISI KUADHIMISHA SIKU YAO MWEZI HUU, JIJINI DAR

Mhandisi Prof. Ninatubu Lema

Na Aron Msigwa – MAELEZO.

Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini imewataka watanzania kutumia huduma za  wakandarasi waliosajiliwa kisheria ili kuepuka kupata maafa na hasara inayotokana na ujenzi hafifu usiokidhi viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (jana)  jijini Dar es salaam mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Ninatubu Lema amesema  kuwa wakati umefika kwa watanzania kuwaamini wahandisi wa ndani kutokana na kazi nzuri zinazofanyika na  hatua kubwa iliyofikiwa katika utoaji wa huduma bora  za ushauri na ujenzi tofauti na kipindi kilichopita.

Amesema katika kuimarisha  na kuboresha huduma za ushauri na ujenzi  nchini Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini kwa kushirikiana na wadau wengine wa taasisi za kihandisi  pamoja na wale wa Jumuiya ya Kihandisi watakutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuoinyesha jamii kile ambacho wahandisi wa Kitanzania wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo nchini.

Ameeleza kuwa hivi sasa kuna wahandisi wengi wanaofanya shughuli za usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu nchini ikiwemo miradi ya barabara , gesi na shughuli za uchimbaji wa madini pia wapo wahandisi wa kitanzania wanaofanya kazi za ushauri katika mataifa mbalimbali ndani na ne ya bara la Afrika.

‘’Kwa upande wetu Tanzania wakati tunapata uhuru tulikua na wahandisi 2 na sasa wako zaidi ya elfu kumi ,jambo hili ni kubwa kwa sababu mchango wa wahandisi sasa tunauona katika kuleta maendeleo ya taifa maana bila ya kuwa na wahandisi vitu vyote tunavyoviona kama barabara, majengo, na miundombinu mbalimbali haviwezi kuwepo”

Prof. Lema amesema maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini yanalenga kuwatambua wahandisi na makampuni  na mashirika ya Kihandisi yaliyotoa mchango mikubwa ya kihandisi katika maendeleo ya taifa na kuwahamasiha wahandisi wengine kufanya shughuli zao vizuri zaidi.

Ameongeza  kuwa maadhimisho yataambatana na tuzo mbalimbali zenye lengo la kuwatia Moyo wanafunzi wahitimu kutoka vyuo vikuu na Taasisi za Uhandisi nchini pamoja na taasisi zitakazotia fora kwenye maonyesho ya ufundi pia kuwafanya vijana washawishike kusomea taaluma ya uhandisi.

Kwa upande wake msajili wa Bodi ya Usajili wa wahandisi Eng. Steven Mlote akizungumzia kuhusu ubora wa majengo yanayoendelea kujengwa kwa wingi jijini Dar es salaam amesema kuwa wamiliki wa majengo hayo wanao mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa majengo yao unazingatia viwango.

Amesema yeye kama msajili anawashauri wamiliki wa majengo kuhakikisha kuwa majengo yao yanayojengwa hivi sasa yanajengwa na wahandisi waliosajiliwa huku akitoa tahadhali kwa wale wanaokiuka kanuni zilizowekwa katika kusimamia ujenzi wa majengo nchini.

“Nawaomba wamiliki wote kuhakikisha kuwa pindi wanapoanza ujenzi wa majengo yao wahakikishe kuwa wanawatumia makandarasi waliosajiliwa, na mtu yeyote anayeruhusu jingo lake kujengwa na watu au kandarasi zisizosajiliwa anakiuka sheria na anastahili kushtakiwa” amebainisha Mlote.

Kwa upande wake Eng. Benedict. Mukama amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuyabaini majengo yote yanayojengwa nchini chini ya viwango na kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya makandarasi wanaohusika na ujenzi wa miradi hiyo huku akieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2011/2012 zaidi ya miradi 164 iliyokuwa inajengwa kinyume cha utaratibu bila kuzingatia viwango ikiwemo ya barabara imesimamishwa.

Aidha amesema maadhimisho haya ya siku ya wahandisi 2012 ambayo yanaadhimishwa nchini kwa mara ya 10 yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kuwa yanawawahusisha washiriki kutoka kutoka nchi za Maziwa Makuu,Afrika ya Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya  kusini mwa Afrika (SADC).